February 16, 2019



KOCHA mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kilichomshinda kwenye mchezo wake ni ubunifu kwa wachezaji kwani walizidiwa maarifa na wachezaji wa Simba.

Zahera amekubali kupoteza mchezo wake wa leo na kuwaweka kiporo Simba mpaka mwakani ili awatungue mabao mengi zaidi.

"Nimeshindwa kuwafunga Simba kwa kuwa walikuwa bora na wachezaji wake wana akili uwanjani, ila mimi sishangai na wala siwalaumu wachezaji wangu wamecheza kwa juhudi licha ya kufungwa leo.

"Nimewaona Simba wakiwa uwanjani walikuwa wanatafuta bao licha ya kuwadhibiti, bado tuna nafasi ya kufanya vizuri michezo yetu ijayo endapo nitapata wachezaji bora ambao ninawahitaji," amesema Zahera.

Mzunguko wa kwanza Simba akiwa mwenyeji alilazimisha suluhu ila leo akiwa mgeni amemfunga mtani wake Yanga bao 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere.

5 COMMENTS:

  1. Asante Zahera Kwa Kubali Yaishe Kwakuwa Sasa Ulisha Kuwa Mchambuzi Wa Soka Na Si Kocha Ila Upo Vizuri Kingine Kilicho Iponza Yanga Pamoja Na Kukosa Ubunifu Pia Acheni Kuwa Na Imani Za Kishirikina Leo Wachezaji Wa Yanga Wa Kikos Cha Kwanza Hawakutumia Usafiri Wao Wa Bas Wali Kodi Coster Kuwapeleka Uwanjani Na Bado Hawakutumia Mlango Sahihi Wa Kuingilia Zote Hizo Ni Imani Za Kishirikina Mwisho Hazijasaidia Chochote Wajifunze Kwa Mzungu Wa Simba Kambi Dar Badala Ya Zanzibar Kama Ilivyo Kuwa Imezoeleka Zamani Achen Kuamini Uchawi Kwenye Soka Gharama Kubwa Za Kambi Morogoro Na Za Mganga Wenu Ni Bora Mnge Wapa Wachezaji Wenu Motisha Kama Simba Inavyo Fanya Saizi Asanteni Simba Kwa Kazi Nzuri Itakayo Fanya Juma Pili Iwe Bomba Sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli mpuuzi ulichangia kiasi gani yanga kwenda moro? Mbona miaka yote simba wanaopenda kuweka kambi!
      Hv kabla ya mechi sio nyie mlisema mtashinda kirahisi lkn kipi kimetokea hilo goli lenyewe kwa mbinde!
      Unajua kabla ya mechi hao wachezaji walipewa kiasi gani? Usiongelee usioyajua

      Delete
    2. Kukubali madhaifu ni moja ya ujasiri na ukakamavu, Kaka JOSEPH, huu mchezo hauhitaji hasira. Hakuna asiyejua kuwa Simba ina kikosi bora na wachezaji bora kuliko Yanga, achana hata na hayo mengine ya posho, mishahara wala uongozi; Simba ina wachezaji bora na kikosi bora kuliko Yanga.

      Hayo mengine ya Ushirikina Yanga mliyachokoza pindi tu baada ya Simba kumfunga Ahly, mkaishutumu Simba kuwa imefanya ushirikina. Hayo mengine ya kupanda Coaster inawezekana ni sehemu ya ushirikina lakini mimi siamini sana maana inawezekana kutokana na hali yenu kiuchumi kuwa sio nzuri, labda mlikosa fedha ya mafuta kwenye basi lenu. Hayo ya Kuingilia mlango usio wenyewe sijui mliamua nini na mnajua fika Kanuni za TFF zinasemaje, natambua Kamati ipo na TFF ipo, hatua zitachukuliwa. Na sijui hofu yenu ilikuwa ni ipi wakati ninyi Yanga ndio mlikuwa Wenyeji na Simba walikuwa wageni!. Poleni sana, huu ndio mpira. Tatizo Kocha wenu aliamini zaidi kwenye "maajabu ya mpira" kuliko ufundi na mbinu.

      Delete
  2. Kuna upuuzi mkubwa sana kuamini ushirikina ukiangalia mechi zetu zote tulizoingia na maimani ya kishirikina tumefungwa au kupata sare Yanga hebu ibadilike tuachane na aibu ya haya mambo, tusajili wachezaji wenye viwango na uwezo na kuwekeza kwenye masilai ya wachezaji,maandalizi, afya na mafumzo

    ReplyDelete
  3. Nina uhakika Yanga safari hii haijapunjwa kitu, imepata sawasawa na mapenzi yake. Yaani Yanga ilistahili walichokipata. Kwaheri Zahera, sina uhakika kama duru la kwanza msimu ujao tutakapokutana na Yanga kama na wewe utakuwepo. Maana naamini hata hapo ulipo kwasasa unajikaza tu. Naamini sasa unaweza ukaanza kutambua Sifa za Kinyonga.

    Nina uhakika washabiki wako huwa unawaona uwanjani wakiwa wamebeba lisanamu la Kinyonga. Sijajua wewe binafsi huwa unatafsiri vipi lisanamu lile. Kama tafsiri yako huwa ni "Polepole ndio mwendo" kwavile kinyonga mwendo wake ni taratibu, unakosea sana. Tabia nyingine ya Kinyonga utaanza kuiona kuanzia baada ya matokeo haya ya kupigwa na Mnyama. Kila la kheri Zahera, usipunguze kuongea, maana kuongea kwako ndiko kunakowapa wapinzani hasira na matokeo yake wanakujeruhi kwa vitendo. Na ukiendelea kujeruhiwa kwa vitendo, hiyo ndiyo furaha yetu Simba. Ubingwa unabaki Msimbazi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic