UONGOZI SIMBA WATOA TAMKO ZITO JUU YA ZANA COULIBALY
George Weah mchezaji pekee kutoka Afrika kushinda Ballon’Dior alipopelekwa Monaco ya france kucheza alibezwa sana mwanzoni na ilibaki kidogo arudi Afrika kama c kocha Arsene Venger!!
Okwi alipokuja Simba miaka ile tulisema viongozi wameleta mvulana wa shule na leo tunamuimba nchi nzima!
Nwakwo Kanu alionekana ngongoti zaid kuliko mcheza mpira kule Ajax ktk siku zake za mwanzo pale Amsterdam!
Hata juzi nilipotoa LINE UP namba mbili ni Zana Coulibaly kelele zilikuwa nyingi sana utadhani mm ndio kocha!
Leo kuna maswali huko kwenu juu ya uwezo wa beki huyu mwenye mbwembwe nyingi?
Nawashauri ndugu zangu c kila mchezaji akija Kwenye Club mpya anaanza vema kama mifano niliowapa huko juu, ni muhimu kuwavumilia na kuwapa uhuru tech bench!
Coulibaly nataka niione mitungi ya kutosha siku zijazo kama jalo la jana ambalo limewafanya waarabu weusi walale saa moja.
Na Haji S Manara
sijaona tamko la uongozi
ReplyDeleteCoulibaly ni bonge ya beki. Nina uhakika mashabiki wa Simba watazidi kumfurahia kadiri siku zinavyoenda.
ReplyDeleteTatizo la Tanzania kila mtu kocha
ReplyDelete