February 15, 2019


UONGOZI wa Simba umemkingia kifua nahodha wa timu hiyo John Bocco kwa kushindwa kutumia nafasi za wazi ambazo anazipata akiwa kwenye mechi za ushindani.

Bocco hivi karibuni katika mchezo wa Ligi Kuu Bara alikosa kutumia vema nafasi tatu alipokuwa na mlinda mlango wa Mwadui FC, pia katika mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Ahly uliochezwa Uwanja wa Taifa Bocco alikosa nafasi mbili za wazi kupachika mabao.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema ni watu wachache wanaoelewa kitu anachofanya Bocco akiwa Uwanjani na kumlaumu anapokosa magoli.

"Wakati mwingine tunapomlaumu kwa kukosa magoli tuangalie shughuli yake kwa mabeki wa timu pinzani, ni mwadamu pekee ambaye amefunga zaidi ya goli mia katika ligi anastahili heshima.

"Amehusika katika kumtengenezea bao Kagere (Meddie) pia bao lake la penalti pale kitwe (Nkana) lilitupa nguvu ya kufuzu makundi, nahodha wangu bora wadhibitishie namna ulivyo, najua utafanya hivi karibuni," amesema Manara.


4 COMMENTS:

  1. Manara aache siasa za kijinga kwanini anaongea kama mtu asiejua mpira? Timu kama timu yaani kwa kizungu team ni mfumo wa watu wengi wanaofanya kazi misili ya kitu kimoja kwa kila mmoja kutimiza majukumu yake aliyopewa ndani ya timu ipasavyo. Sasa John Boko ni mshambuliaji tena ni nahodha na katika migaio ya mpira ya nafasi za kufunga kutoka kwa watafutaji wa nafasi za kufunga yaani midfielders yaani viungo washambuliaj kwa simba mtu wa kwanza wanaetakiwa kumtupia pasi ya wisho iliopatikana baada ya kazi ngumu ya kuitengeza basi ni John Boko .Boko ni mshambuliaji namba moja kwa Simba hivi sasa sio kwa uwezo bali kimajukumu na kazi yake kubwa ni kufunga magoli kwisha habari. Na kama John Boko akishindwa kutimiza jukumu lake hilo ipasavyo basi ajue ana mapungufu amabayo yanaigharimu timu yake kufanikisha malengo yake kwa hivyo ni vyema akajirekebisha na kwa mwanadaamu anaejitambua basi ni vizuri kuchukua jitihada za kujirebisha mwenyewe kuliko kuja kurekebishwa.

    ReplyDelete
  2. Mpira unazungumzia wewe ni mfumo wa kizamani sana.Mpira wa kisasa mshambuliaji ana majukumu mengine licha ya kufunga .Anatakiwa asaidie kujilinda,kutoa pasi.
    Mambo ya namba 9 kusimama kuletewa mpira hamna tena.

    ReplyDelete
  3. Namuunga mkono Manara, Boko ana mapungufu hayo ya kukosa umakini, na ninakubali kuwa Boko ni bonge la Straiker, na pia nakubali kuwa Boko ni mpambanaji. Lakini kama nilivyoweza kumlaumu mara nyingi huko nyuma, anatakiwa kuwa na utulivu na kufikiria zaidi ya kitu kimoja cha kufanya pindi anapokuwa ana kwa ana na golikipa pinzani.

    Maana aina ya magoli yote hayo matano (matatu [3] dhidi ya Mwadui, na mawili [2] dhidi ya Ahly), aliyakosa kizembe, na yote ni ya namna moja. Anashindwa kufikiria namna nyingine ya kumkwepa kipa pinzani, yeye anachowaza ni kupiga tu, bila kuangali kipa anakujaje.

    Nami naungana na Manara kwamba, "Najua siku si nyingi atauonyesha uwezo wake wa kujiamini na kuwa na maamuzi zaidi ya moja na kufuta makosa yake yote hayo".

    ReplyDelete
  4. Boko si mchezaji anaeweza kwenda nje ya nchi kucheza, uwezo wake ni ligi ya Tanzania. Hana uwezo wa kupiga, poor control, poor possession, poor heading,poor accuracy. Ili afunge goli anahitaji attempts 10. Tusifie vinavyosifika.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic