February 15, 2019


KOCHA mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa miongoni mwa mbinu ambazo amewafundisha wachezaji wake ni kupoteza mpira pamoja na kutumia mipira ya adhabu.

Yanga ambao waliweka kambi mkoani Morogoro na baadaye Zahera akaamua kikosi kirejee Dar, ataikaribisha Simba Uwanja wa Taifa baada ya mchezo wa awali Simba kuwa mwenyeji.

"Nimewafundisha wachezaji wangu namna ya kupoteza mpira wakiwa uwanjani, ni mbinu itakayowasaidia wazidi kuwa makini na wautafute mpira pale ambapo wanaupoteza kwenye mechi, pia nimewafundisha namna ya kutumia vema mipira ya adhabu eneo la hatari.

"Najua mchezo utakuwa mgumu ila kwa mbinu ambazo nimewapa nina imani watapata matokeo, ninaamini uwezo wa wachezji wangu na kila kitu kinawezekana," amesema Zahera.

Yanga ni kinara wa Ligi Kuu Bara kwa sasa akiwa amecheza michezo 23 ana pointi 58 huku mpinzani wake Simba amecheza michezo 15 anashika nafasi ya 4 akiwa na pointi 36.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic