February 17, 2019


Uongozi wa klabu ya Yanga umekubali matokeo ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Licha ya kupoteza mechi hiyo, Yanga wameeleza kuwa haina maana kufungwa na Simba ndiyo wamepoteza mbio za ubingwa kwani bado mechi zinaendelea.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema hawajapoteza ligi bali wamepoteza mechi pekee, na haya ndiyo aliyoandika.


2 COMMENTS:

  1. Angekuwa ana chembe ya aibu angenyamaza .Huyu msemaji wetu ni dhaifu kweli kweli.Yeye baada ya kuhamasisha wapenzi waje uwanjani anapiga domo tu.
    Ni aibu kubwa kwa timu yetu ya Yanga kuwa wenyeji lakini kuzidiwa washangiliaji na Simba ambao kwenye mechi ya jana walikuwa wageni.
    Sijui analipwa kwa kazi gani?

    ReplyDelete
  2. Hiyo ndio Yanga bhana! Wakati Da Boss wetu alipokuwa anawahamasisha washabiki wa Simba kufika uwanjani, wakaanza kusema "ooh anawajaza vichwa wachezaji, wanajiamini kupitiliza ndio maana wanafungwa", na zaidi ya hapo mkawa mnamtukana hovyo msemaji wetu. Leo hii mmeona kuwa kazi mojawapo ya msemaji ni kuhamasisha washabiki kuingia uwanjani!, leo hii mnamlaumu Ten wenu!. Haya bhana, Hii ndiyo Yanga yenu bhana, ila sisi tunasema THIS IS SIMBA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic