February 17, 2019


ZANA Coulibaly wa Simba amewazidi kete mastaa wa Yanga, Haruna Moshi ‘Boban’ na Mohammed Issa ‘Banka’.

 Wachezaji hao wote walisajiliwa kwenye dirisha dogo isipokuwa Banka alisajiliwa dirisha kubwa ila alikuwa na adhabu aliyopewa na Shirikisho la Soka la Dunia (Fifa) kwa muda wa miezi 14 adhabu ambayo ameimaliza.

Kwenye mechi ya jana ya watani, Zana ndiye
alianza kwenye kikosi cha kwanza huku
Boban na Banka walianzia benchi kuusoma mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ndani na nje ya uwanja.

 Katika hatua nyingine, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harison Mwakyembe jana aliingia na staili yake uvaaji wa aina yake kwenye mechi hiyo kwa shati lake lilikuwa na rangi ya njano na nyekundu

3 COMMENTS:

  1. Mimi bado najiuliza kwanini vijana wetu wa kitanzania baadhi yao wanakuwa wazembe kupitiliza kiasi. Hapa ninamzungumzia Adama Salamba. Unaona kabisa ulimbukeni na kujifanya yeye bishoo wa mjini ndicho kinachomfanya Adam Salamba kupotea. Ukisema hapewi nafasi pale Simba kuonesha uwezo wake basi ni uongo. Nafasi anapata kuonesha uwezo wake lakini hakuna anachokionesha. Mfano mashindano ya mapinduzi cup kule Zanzibar. Yale mashindano yalibeba hatima ya namba ya Salamba ndani ya kikosi cha kwanza cha simba lakini cha kushangaza Salamba wa mapinduzi cup alikuwa Salamba wa hovyo kupita maelezo. Yakaja mashindano ya sport pesa haya yote ni mashindano amabayo Salamba alitakiwa kuonesha ubora wake lakini kilichotokea ni bure kabisa. Kombe la FA Simba inalaumiwa kutolewa kizembe na timu ya mchangani ila haya yote ni mashindano yaliokuwa yakitoa nafasi kwa akina Salamba kuonesha uwezo wao lakini hakuna walichokionesha na mzungu huwa hanaga figisu sijui ampange mtu kwa kuwa anamahaba nae binafsi hapana siku zote wao hutizama uwezo wa mtu hasa anapompa nafasi mchezaji wake ya kucheza siku zote huwa wanataka kuona juhudi ya dhati kutoka kwa mchezaji husika na ndio maana Nicholasi gayani kuna hatari ya kuisahau nafasi ya beki mbili kutokana na uwezo wa kujituma wa zana coulibali. Salamba bado ana nafasi kwenye fowadline ya Simba kama angelikuwa ni kijana anaejitambua na wala Simba isingehangaika kuleta wahambuliaji wa majaribio mbele ya macho yake. Mchezaji ukiona timu yako inahangaika kutafuta mchezaji wa nafasi yako unayocheza utajisikia vipi? Hufai,huna maanana, timu walishajiridhisha kuwa mchezaji alikuwepo hatoweza kuwasaidia wala hana dalili ya kuimprove huyo ndio Adam Salamba wa Simba. Muangalie kagere anavyohaha uwanjani,muangalie Okwi anavyohaha uwanjani, hawa wote ni wachezaji walishacheza mpaka ulaya na baadhi ya club kubwa Africa kama watu wa kuridhika au kufanya ubishoo na kujiona pale simba wangekuwa wachezaji hawa au chama sio Adam salamba! Ndipo pale tunapoona watanzania tuna matatizo makubwa hatuna malengo wala hatujali majukumu yetu ya kazi. Wala vijana hawafundwi jinsi ya ujasiri kazini kufanya mambo makubwa. Ningemuomba tu Adam Salamba na vijana wengine nchini yakwamba maisha ni kufanya kazi na kazi ni vita isiopoa kutokana na ushindani wa ajira wa kila mmoja kutaka kuwa bora zaidi kuliko mwenzake na kama vijana wetu wataendelea kuwa watu wa kujilegeza tu basi hakuna hata mmoja atakaetimiza ndoto ya kutaka kutoka kwani huko ulaya au nje ya Tanzania ushindani wa namba ni wa balaa zaidi bila ya konesha jitihada za ziada si rahisi hata kidogo kukubalika na wageni utarudishwa tu ulipotoka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hoja zako ziko vizuri.Ni kweli asilimia kubwa vijana wetu hawajitambui na malengo yao ni kama wanafanya mdhahaa.

      Delete
  2. Alianza kujifanamisha na Ronaldo mara tu aliposajiliwa simba. Nikaona lazima atapotea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic