Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutoka kundi la WCB Wasafi, Harmonize anashikiliwa kwa zaidi ya saa tano katika Kituo cha Polisi Central, jijini Dar es Salaam alipokwenda kujisalimisha akituhumiwa kuvuta bangi alipokuwa nchini Ghana.
Muimbaji huyo ameitikia wito wa RC Makonda, ambaye alimtaka akifika nchini achunguzwe kuhusiana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi baada ya kuonekana akivuta kitu chenye moshi mkubwa kinachodaiwa kuwa ni bangi.
Makonda alisema alimwagiza Gavana wa kule amchunguze alichokuwa akivuta na kama ikithibitika kilikuwa na kilevi angemwajibisha.
Harmonize leo alijisalimisha katika kituo hicho akiwa amejifunika kichwani kwa kuvaa sweta jeusi na miwani.
Alipofika kituoni hapo alitimua mbio huku akiwafurusha waandishi waliokuwa wakijaribu kumpiga picha.
0 COMMENTS:
Post a Comment