BODI YA LIGI YAWAJIBU NAMNA HII YANGA KUHUSIANA NA RATIBA
Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania, Boniface Wambura, amesema kuwa ligi ilipofikia imebanana kiasi cha baadhi ya timu kutofautiana idadi ya mechi walizocheza.
Wambura ameeleza kuwa kumekuwa na mashindano mengi hivi karibuni ambayo yamesababisha ratiba hiyo kupangwa na kupanguliwa hivyo mechi kushindwa kwenda kama ilivyokuwa imepangwa awali.
Kauli ya Wambura imekuja mara baada ya Kocha Mkuu wa Yanga kuutumia lawama uongozi wa TFF kuwa wanaionea Yanga kwa namna ambavyo ratiba hiyo inakwenda hivi sasa.
Kiongozi huyo amesema hakuna namna kwa vile kulikuwa na muingiliano wa mashindano ikiwemo Simba ambayo inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kucheza mechi chache mpaka sasa.
"Ni kweli ratiba imebanana zaidi hivi sasa ukiangalia kulikuwa na mashindano mengi ambayo yalileteleza kupangwa na kupanguliwa kwa ratiba, tunapambana kwa namna tuwezavyo ili kila kitu kikae vizuri" alisema Wambura.
TFF acheni kuwasikiliza sana hawa Yanga, tayari maji yamewafika shingoni kutokana na kuanza kutoka nje ya Dar na kupata matokeo ambayo hawakuyatarajia kuyapata. Hayo ni malalamiko tu yasiyo na tija, mnadhani kama Yanga wangeshinda Tanga na jana Singida wangetoa malalamiko kama haya? Wao wanajiona kama ni Miungu ya ushindi tu. Lazima wakubaliane na matokeo bhana, ratiba ni ngumu kwa timu zote, sio Yanga pekee, kwanini walalamike wao tu! au kwavile mbao hawana wa kumlalamikia, au kwa vile Biashara hana wa kumlalamikia! Mzunguko wa kwanza timu kama Biashara karibu zaidi ya nusu ya mechi 19 walicheza nje ya Musoma, na walipoteza mechi karibu zote na kutoa sare kutokana na kucheza nje ya kwao, hawakulalamika, iweje hawa Yanga walalamike sana! Au wanataka TFF wafanye kama wanavyotaka wao!!?. Na bado. Yaani hapa mechi 5 mnachukua pointi 3 tu!
ReplyDeleteNyinyi mlikalili upande mmoja wa shilingi, tumehamia upande wa pili wa shilingi sasa, kubalianeni na kila takwa la upande huu wa pili wa shilingi. Kulalamika sana hakuwezi kuwaponya, zaidi niwashauri tu anzeni kuimba mapambio ya niagieni.
DeleteHizi hapa ratiba za Simba na Yanga kwa mwezi huu Februari 2019
ReplyDeleteSIMBA SC
��07/02/2019
Simba vs Mwadui - Dar
��12/02/2019
Simba vs Al Ahly - Dar
��16/02/2019
Yanga vs Simba - Dar
��19/02/2019
Africa Lyon vs Simba - Arusha
��22/02/2019
Azam vs Simba - Dar
��26/02/2019
Lipuli vs Simba - Iringa
��03/03/2019
Stand United vs Simba - Shinyanga
��09/03/2019
Js Saoura vs Simba - Algeria
��16/03/2019
Simba vs As Vita - Dar
��18/03/2019
Simba vs Ruvu Shooting - Dar
��31/03/2019
Simba vs Mbao - Dar
YANGA SC
��06/02/2019
Singida United vs Yanga -Singida
��10/02/2019
JKT Tanzania vs Yanga -Tanga
��16/02/2019
Yanga SC vs Simba -Dar
��20/02/2019
Mbao vs Yanga -Mwanza
��25/02/2019
Namungo vs Yanga -Lindi
��02/03/2019
Alliance School vs Yanga Mwanza
��10/03/2019
Yanga vs KMC -Dar
��16/03/2019
Lipuli FC vs Yanga -Iringa
March 25-30 ASFC robo fainali
NANI HAPO ANA NAFUU ? AFADHALI YANGA RATIBA YAKE INA SIKU ZA KUPUMUA KULIKO SIMBA. TUCHEZENI TUU HIYO NDIYO LIGI HAKUNA KULALAMIKA
Delete