February 11, 2019



UONGOZI wa Simba umesema kuwa umejipanga kiusahihi kuhakikisha wanatimiza ahadi yao ya kubakiza pointi tisa za nyumbani katika michezo ya Ligi ya Mabingwa ambayo itachezwa walianza na JS Saoura na sasa ni zamu ya Al Ahly ya Misri.

Smba inatarajiwa kucheza na mwarabu wa Misri Al Ahly Kesho Uwanja wa Taifa saa 10:00 jioni ambapo kiingilio kwa jukwaa la mzunguko ni shilingi elfu mbili tu.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema wanatambua mashabiki wengi wana maumivu hasa baada ya kushindwa kufanya vizuri katika michezo yao miwili ya ugenini sasa ni muda wao wa kulipa kisasi.

"Tunajua namna gani ambavyo mashabiki wanaumia kutokana na matokeo mabaya ambayo tuliyapata Misri, ila tuna nafasi ya kufanya vizuri na kupata matokeo kikubwa ni wana Simba kuungana na kuishangilia timu yetu.

"Mwaka 1985 tulikutana na mabingwa hawa katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na tuliwaua waarabu kwa mabao 2-1 tena wakati huo ilikuwa ni moto wa kuotea mbali zaidi ya sasa kama iliwezekana wakati ule kwa nini jumanne isiwezekane?, Yes we Can," amesema Manara.

5 COMMENTS:

  1. Kabisa mpira sio maneno ni vitendo. Cha msingi Simba na wachezaji pamoja na benchi lake la ufundi wakubali kufuata ushauri wa kiufundi unaotolewa na wadau mbali mbali. Suala moja la msingi amabalo wachezaji wa Simba wanapigiwa kelele ni umakini na kujitolea. Umakini wakati wote wa mchezo lakini hasa katika dakika za mwanzo za mchezo mpaka kuishia kipindi cha kwanza kwani ni mikakati maalum ya timu za kaskazini mwa bara Africa hasa El Ahly kuwamaliza wapinzani wao katika kipindi hicho. Kukosa kujitolea kwa wachezaji wa Simba kwa kweli ni moja ya tatizo kubwa kwa wachezaji wa Simba. Wanatakiwa kujituma kuonesha thamani ya jitihada yao ya kufika hapo walipofikia sasa.katika mechi iliyopita wachezaji wa Simba hawakuenda kushindana kule Misri bali waliingia uwanjani kuwatizama Ahly jinsi wanavyocheza mpira yaani wachezaji wa Simba walikuwa watazamaji walioingia bure uwanjani kwa kweli wanapaswa kubadilika.lakini licha ya wadau kupaza sauti zao kuwataka wachezaji wa Simba kubadilika lakini inaonekana kana kwamba wanaoshauriwa wametia pamba masikioni hawasikii. Vile vile bila shaka katika game iliyopita kati ya Simba na Ahly kule Misri kulikuwa na key players au wachezaji waandaamizi kama sio waangamizi waliokuwa na madhara zaidi kwa upande El Ahly. Wachezaji hao wanatakiwa kuchungwa sana muda wote pamoja na kudhibiti maeneo yao muhimu waliyoyatumia kuimaliza simba katika mechi iliyopita. Katika mechi na As vita Simba ilionywa kuwa makini na badhi ya wachezaji ambao simba wakizembea kuwakaba basi watajuta na walitajwa kwa majina cha kushangaza na mshangao wa wengi ni wachezaji haohao ndio waliokuja kuimaliza simba kiulaini kabisa ndipo pale mtu unapojiuliza Simba
    tatizo sio la wachezaji tu bali tatio la Simba kutofanya vizuri linaanzia kwenye safu ya uongozi,benchi la ufundi na kuishia kwa wachezaji sasa lazima tubadilike nashukuru Mwenyekiti Mo kaliona hilo. Simba ipo katika kipindi cha maboresho kwa sasa kama alivyokwishakusema Mwenyekiti Mo kuwa ni kipindi kwa Simba kuutafuta ubora halisi wa Simba sio Simba jina tu, kutafuta wafanyakazi wanaojali kazi yao pengine sio kujali tu bali wanaoipigania kazi yao kwa maslahi mapana ya klabu yaani wachezaji wanaoonesha jitihada ya kuipigania timu kwa nguvu zao zote. Simba ni timu kubwa,Simba ilioyomtoa samata sio brand ndogo hata kidogo . Cha kushangaza wachezaji wa Simba wanashindwa kulitambua hilo hata kwa kujitangaza wao wenyewe binafsi kwa sifa ya kujitoa. Ukiwaangalia wachezaji wa simba waalivyo sasa kitabia kama vile wapo kwenye timu ya mitaani? Simba ni kampuni Simba ni professional team na wanasimba tunaamini mabadiliko ya mpira wa Tanzania yatakuja kutokana na mabadiliko ya dhati ya kimkakati ya kimaendeleo ya Simba na inawwzekana. Kwanini Simba? Simba ina hazina kubwa ya rasilimali watu wa kuiwezesha kufikia malengo makubwa kabisa. Ukiachana na Mo na akina kibadeni.Watu kama akina Twalibu Hilali,Khassani Afif nakadhalika ingawa baadhi yao wapo mbali lakini kama jitihada zitanyika za kuwashirikisha japo kutoa ushauri wao basi wanaweza kutoa mchamgo mkubwa kabisa wa kuisadia timu kupiga hatua. Kwa hivyo kwa kiasi kikubwa mechi ya jumanne kwa Simba ni mechi ya kujitasmini kwa kila mwana Simba na katika kujitasmini huko lazima kuanze kwetu sisi wapenzi,mashabiki na wanachama wa Simba kwanza kwa kiasi gani tutajitolea kwenda kuisapoti timu yetu. Vile vile ni wakati muafaka wa kwenda kufanya tasmini kwa wachezaji watu kiasi gani wamebadilika baada ya kelele na vilio vyetu nyingi tulivyovipiga kutaka wabadilike. kwa hivyo Siku ya jumanne ni siku ya kwenda kujionea wenyewe na kuipa sapoti timu,tukutane kwa mchina.

    ReplyDelete
  2. Pamoja na wachezaji kukosa kujituma hata hisabati za mwl ni kikwazo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic