WAWILI WAENGULIWA YANGA
Wachezaji wa Yanga Kiungo Feisal Salum Feitoto na beki Gadiel Michael wataikosa mechi ijayo ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC, Jumatano ya February 20 2019 katika dimba la CCM Kirumba Mwanza.
Wawili hao watakuwa nje ya dimba kutokana na kuwa na kadi tatu za njano hivyo kwa mujibu wa sheria za soka itawabidi kutohusika kwenye mechi hiyo.
Tayari kikosi cha Yanga kimeshafika jijini Mwanza na jioni ya leo kitaanza amzoezi kuelekea kipute na Mbao Jumatano ya wiki hii.
Yanga itakuwa inaenda kucheza mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Simba kwa kufungwa bao 1-0 jijini Dar.
WA 3 NI SIMON GUSTAV
ReplyDelete