February 18, 2019


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema yupo tayari kufanya kazi klabuni hapo bila malipo, imeelezwa.

Taarifa imeeleza kuwa Zahera ameshawahi kufanya kazi sehemu tofauti bila kutegemea malipo hivyo haoni tatizo kwake endapo akifanya hivyo Yanga.

Zahera ambaye amewahi kusema timu yao inapitia wakati mgumu, ameeleza kuwa amekuwa akitoa hata fedha zake kwa ajili ya kuisaidia klabu haswa kipindi hiki cha mpito.

Kocha huyo amefunguka kuwa hategemi mshahara kuendesha maisha yake kwani ana biashara nyingi ambazo anazifanya.

Kwa moyo huo, Zahera ana imani kuisaidia Yanga kutaongeza morali kwa timu na wachezaji kwa ujumla kwani mshahara kwake si ishu na yupo tayari kufanya akzi hiyo bila kulipwa kwa miaka mingi.

7 COMMENTS:

  1. Anawapa Mkwara Yanga Ambao Hawana Hela Na si Anajua Aliahidi Kuifunga Simba So Alipo Shindwa Ameamua Kwawapa Mkwara Mzito Wapenzi Wa Yanga Yaani Zahera Kwa Ufupi Ni Mbinafsi Maana Anajipraudi Sana Kazi Yake Ni Kuchambua Chambua Utazania Yeye Ndo Yeye Hakuna Mwengine

    ReplyDelete
    Replies
    1. we bwege hujui mpira ndo mana unaongea hizo pumba.....tafuta wana simba wengine wanaojua mpira au mtu yeyote hawawezi anaejua mpira hawezi kukuambia kuwa zahera sio kocha mzuri.

      Delete
  2. Amekuwa maarufu kuliko klabu.... hahhahhaa...anaficha udhaifu wake ipo siku atagundulika tu na ndo utakuwa mwisho wake.

    ReplyDelete
  3. Zahera Papaa ni kocha mzuri tu,kufungwa na mikia kwa kipindi hiki ni sahihi kulingana na changamoto zilizopo ndani ya Club,kikosi cha Mikia ni kizuri kuliko cha Yanga,huo ndio ukweli.
    Kitu cha msingi mashabiki tuendelee kusapoti timu yetu,bado tuna nafasi ya kubeba ubingwa,tusichukulie uzuri wa kikosi ni kuifunga simba pekee...
    "Daima Mbele......."

    ReplyDelete
    Replies
    1. Changamoto ni visingizio tu!walishaingiza hela nyingi kwa kucheza nyumbani...Kuna hela wanapata sportpesa..kuna hela ya mashibdano CAF mwaka Jana!Vodacom na kopo kutembezwa.Hivi changamoto za Yanga ni walikuwa na madeni makubwa au ni visingizio tu!Hata juzi wamepata mil 165 asante kwa washabiki wa mikia walienda uwanjani kwani wa vyura waliamua kubaki matopeni.wasingeenda wa Simba Yanga ingeishia pata mil kama 70 hivi!

      Delete
  4. Huyo yanga hawatomwacha hata wakiendelea kufungwa kwakuwa wana kocha wa bure na wanahisi yatasaidia kuwafanya wachezaji wasidae haki zao na waendelee kujikaza kisabuni lakini subira pia in mipaka na yeye Zahera anasema hana haja ya mshahara kwakuwa anazo lakini vipi hao vijana?

    ReplyDelete
  5. Ameona mbele ni kuzito kutetea kibarua chake, hivyo ametanguliza mkwara ili wanaYanga waamini kuwa hata wakimfukuza watakuwa hawajamkomoa kwakuwa hategemei kazi ya ukocha pekee kwenye maisha yake. Hiyo ni hali ya kujilinda kibinafsi (Personal Diffence).

    Ila kwa upande wa pili ameshindwa kuangalia kuwa wanaomuweka pale ni vijana (ambao ni wachezaji), wale maisha yao ni mpira na mpira ndio maisha yao. Je, atatumia rasilimali zake hizo kama alivyoeleza "nina biashara nyingi" kuwasaidia na hawa vijana?. Maana sawa yeye hatalipwa mshahara kulingana na hali ya timu, ataendesha maisha yake kwa biashara zake, je hawa vijana waliojiajiri kupitia mpira?!.

    Atoe ahadi basi ya kuwalipa mshahara au kusaidia kuchangia mishahara ya hawa vijana.

    Binafsi naona anajilinda tu yeye binafsi kupitia kibarua chake. Angeona biashara zake zinamtosha katika maisha yake, asingeacha familia yake huko kwao akaja kupigizana makelele na kulalamika kila siku mashabiki wa Yanga wanamtukana.

    Na utetezi huo unakuja baada ya kujipa na kuwapa wanaYanga Imani kubwa ya kuifunga Simba. Sasa amepigwa yeye, matokeo yake ndo haya. Atakuwa keshaambiwa tu na wanaompenda kuwa hapa Bongo ukiwa Kocha wa Simba ukifungwa na Yanga ujue safari ya kurudi kwenu inakuhusu, na pia ukiwa kocha wa Yanga kisha ufungwe na Simba vilevile safari ya kwenue inakuhusu. Sasa Zahera yamemkuta, anahisi safari hii ni ya kwake, hivyo anajilinda kwa kujipa imani kuwa hata wakimfukuza hatakuwa na cha kupoteza kwakuwa ana biashara nyingi za kumuendeshea maisha yake.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic