February 17, 2019


BEKI Kelvin Yondani jana kwenye mechi yao na Simba alikataaa unahodha baada ya nahodha mkuu, Ibrahim Ajibu kutolewa. Sekeseke la mastaa hao wawili lilianza kuonekana wakati wachezaji wakisalimiana kabla mechi haijaanza ambapo Yondani aligoma kumpa mkono Ajibu hata alimpomsubiri kwa sekunde kadhaa.

Kama hilo halitoshi, Yondani alikikataa kitambaa cha unahodha baada ya Ajibu kutoka, Ajibu alimpa Fei Toto akampe Yondani lakini yeye akamuonyesha akampe Ngassa ambaye ndiye aliyekuwa nahodha baada ya Ajibu kutolewa.


Yondani alivuliwa unahodha wa timu hiyo mapema Januari mwaka huu baada ya kuonyesha nidhamu mbovu. Nahodha Msaidizi wa Yanga ni Juma Abdul ambaye jana hakucheza.

Lakini katika mchezo huo, Yondani ndiye alikuwa akizungumza na refa mara nyingi kuliko Ajibu nahodha na niye aliyekuwa jukumu la kuongea na mwamuzi.

Yondani alizungumza na refa katika matukio ya faulo ya Okwi dk 10, faulo ya Tambwe dk 12, faulo ya Boxer dk 14. Pia Yondani alikuwa akiwapa maelekezo kila mara wachezaji wenzake hasa Ninja, Dante na Gadiel.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic