YANGA WAANZA FITINA NJE YA UWANJA
BAADHI ya wanachama kutoka matawi ya Yanga Temeke, yamepanga kukutana haraka, kupanga mbinu za nje ya Uwanja zitazoisaidia timu yao kupata ushindi dhidi ya Simba mchezo utakopigwa jumamosi hii Uwanja wa taifa.
Yanga watawakaribisha Simba Jumamosi hii, kwenye mchezo wa ligi kuu bara utakaopigwa Taifa, ambapo Yanga atakuwa anatafuta alama tatu ili ajichimbie kileleni, huku Simba nao wakitaka pointi hizo hizo tatu ili waweze kurudi kwenye mbio kutetea taji lao.
Akizungumza na Spoti Xtra,mjumbe wa tawi la Yanga Mbagala Kibondemaji, Lilian Lukindo alisema; “Tumepanga kukutana wanachama wa matawi yote kutoka Temeke ili tujadiliane mbinu za nje ya Uwanja zitazoisaidia timu yetu kupata matokeo mbele ya Simba.
“Kwa sababu siku zote mashabiki ni mchezaji wa tatu kwahiyo lazima tujipange vizuri kuelekea mtanange huo,”alisema Lukindo.
0 COMMENTS:
Post a Comment