February 15, 2019


MBELGIJI wa Simba, Patrick Aussems amesikia kelele za Yanga kwenye mitandao akacheka halafu akatikisa kichwa huku akichezea kidevu chake.

JUMAMOSI ijayo Uwanja wa Taifa kutakuwa na mchezo wa watani wa Jadi. Simba wao watakuwa kwenye kazi mpya ya kumtafuta atakayeamua matokeo kutokana na nyota wao Shiza Kichuya kupata timu ya kucheza msimu huu nchini Misri ya ENPPI inayoshiriki Ligi Kuu.

Kichuya alipokuwa na Simba alikuwa na uwezo wa kuamua matokeo wakati Simba ikiwa nae stori kambini kwenye hoteli ya Seascape eneo la ufukwe wa Mbezi,unajua alichosema?

“Kama nimeweza kumpiga Al Ahly mwenye kikosi cha Mabilioni pale Taifa, Yanga anachomokaje?” Kocha huyo amesema mchezo huo ni rahisi sana kwake wala yeye na wachezaji wake hawana
presha hata chembe.

Anaamini kwamba mechi na Ahly ndiyo ilikuwa kipimo cha kuivaa Yanga. Aussems ameweka wazi kwamba katika mchezo huo wa Jumamosi mashabiki wa Simba kwa mara ya kwanza watamuona kwenye benchi kocha wake msaidizi. Licha ya kwamba hakumtaja kwa jina lakini Spoti Xtra linajua ni Denis Kitambi aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Azam.

Jana Alhamisi Kitambi alianza kazi rasmi baada ya kusaini mkataba juzi jioni na muwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji ‘Mo’.

“Nimekuwa nikifanya kazi kwa miezi miwili sasa lakini sikuwa na msaidizi lakini kwa sasa nimepata bado tu kukamilisha taratibu na kama mambo yatakwenda sawa ataingia mkataba na kuweza kuanza kazi
kama ambavyo unajua kwa sasa tuna majukumu.

“ Nimemuona ni kocha mzuri ambaye nitaweza kufanya naye kazi hivyo sina tatizo katika hilo cha msingi ni sisi kuweza kuelewana na kufanya kazi kwa pamoja kama kawaida bila shida yote,”alisema Kocha huyo.

Kwa upande mwingine kocha huyo alisema; “Kipimo chetu kikubwa kuelekea mechi ya Yanga ilikuwa ni mechi ya Ahly ambayo tumefanikiwa kupata matokeo hivyo sasa nguvu zetu na maandalizi yanaendelea vizuri bila presha kuelekea mechi na Yanga.”

“ Na mechi hii hatuna presha sana kwa kuwa ni mechi kama ilivyo mechi nyingine za ligi kikubwa ni kujiandaa na kuona vipi timu inapata matokeo bila tatizo.

“Ingawa watu wengi wanaichukulia mechi hii kitofauti na kuonekana ukubwa huku ikiwa ni mechi kama zilivyo nyingine cha msingi ni kuondoka na pointi tatu ilikuweza kuona tunatetea ubingwa wetu wa ligi kuu, ”alisema Patrick.

CHANZO: CHAMPIONI

4 COMMENTS:

  1. Simba hawatakiwi kuichukulia mechi na Yanga kimzaha mzaha kwani licha ya Simba kuifunga Alahly bado wanasimba wangali wamegandwa na jinamizi la hamsa hamsa za Congo na Misri. Simba mechi yao na Yanga ni mechi muhimu sana tena sana mechi ambayo kwa Yanga kama wanavyosema ni mechi itakayowahakikishia ubingwa kwa hivyo utaona kwa jinsi gani yanga walvyojidhatiti. Simba ilikuwa haina haja yakwenda Zanzibar au pemba kujiandaa na Yanga kwani safari ya Congo na Misri pamoja na pambano lao la mwisho na Alahly basi ni maandizi tosha ya kujua mapungufu yao yapo wapi ila kama Simba watajituma kwa pamoja kama walivyofanya dhidi ya Alahly basi Yanga kazi wanayo.kama Simba walipata somo la kufungwa goli tano mara mbili kwanini wasiichukulie mechi ya Yanga na wao wakatoa somo hilo la hamsa kwa mtani na kukata kidomodomo cha hamsa hamsa mitaani.

    ReplyDelete
  2. Nimependa sana kocha anavyoichukulia hii mechi hii,anaichukulia kama ya kawaida na hii itawaondolea presha wachezaji na hivyo kucheza kwa kujiamini, kisaikolojia ni nzuri sana kwa wachezaji cha msingi wasibweteke tu wacheze kwa uwezo wao wa kawaida na watashinda kirahisi sana.

    ReplyDelete
  3. Mim Sina Presha Na Yanga Najua Mchezo Utaisha Kipindi Cha Kwanza Tu Na Kesho Hiyo Nitakua Wa Kwanza Ku Comment Kweye Blog Hii Kama Tukifungwa Itakua Bonge La Aibu Kubwa Kwa Jins Kikos Kikosi Kilivyo

    ReplyDelete
  4. Nimefurahi kupatikana kwa kocha msaidizi. Ausems alishaelemewa na majukumu, ni heri sasa amepata msaada.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic