February 18, 2019




MWINYI Zahera amesema kuwa kisasi chake dhidi ya Simba bado kipo anaanza maandalizi sasa ili kuwanyoosha katika msimu ujao endapo watakutana kwenye Ligi Kuu Bara.

Mbinu za Zahera zilizidiwa na mbelgiji wa Simba Patrick Aussems kwenye mchezo wao wa marudio dakika ya 71 Uwanja wa Mkapa baada ya wachezaji wake kufanya makosa yaliyoigharimu timu yake na kuruhusu kufungwa bao 1-0.

"Nimefungwa ni kweli sikuwa na namna maana wachezaji wangu mbinu walizidiwa ila kama ambavyo mnaona hakuna namna nyingine yoyote ya kukifananisha kikosi changu na wapinzani wangu.

"Nawaambia wazi kama ambavyo nimekuwa nikiwaambia, mwakani hawa watanitambua nina amini nitalipiza kisasi hiki kwani kwa sasa wachezaji nilionao wengi asilimia kubwa sio wale ambao niliwachagua mimi," amesema.

Yanga wamepoteza michezo miwili kati ya 23 waliyocheza kwa sasa ambapo walianza kupoteza mbele ya Stand United na mchezo wao wa pili ni dhidi ya Simba.

6 COMMENTS:

  1. Huyu nae, anafikiri msimu ujao na simba hawatafanya usajili wa maana, na je yanga watapata hela ya kusajili hao wachezaji atakoa? mi naona ataendelea kuteseka tu, simba wako vizuri kiuchumi na kimipango.

    ReplyDelete
  2. Sifa zote kwake kwasababu ameweza kujenga kikosi imara pamoja na kuwa usajili wa Ynaga kwa misimu miwili ni wa chini sana!

    ReplyDelete
  3. Na asajili wa kuwasajili ikiwa bakuli litakuwa na uwezo wa kuleta nyota kama wale wa Simba ambapo pia Moo keshatamka kukifumuwa kikosi upya na kukijenga tena upya. Wakale wamesema kuwa mkono mtupu haurambwi na ukiona vinangara vimeundwa. Mwaka huu wa nwanzo, Moo aliuona wa majaribio ili ajuwe hasa nini kinachotakiwa. Ukenda hatuwa moja Moo atakwenda kumi

    ReplyDelete
  4. Kwanza anategemea huo msimu ujao ataweza kuufikia akiwa Yanga!. Na pili, kwenye ile sare ya mzunguko wa kwanza alisema mechi ya marudiano mtanitambua, nitakuja kivingine. Na akarudia tena siku mbili kabla ya mechi kwa kusema kuwa, safari hii tutaiona Yanga nyingine, sio ile iliyocheza na Simba mzunguko wa kwanza.

    Hivyo, huyu jamaa anajaribu kucheza na Saikorojia za watu tu, hana jipya. Anadhani kwamba yeye akifanya usajili wa maana kwa wachezaji anaowataka yeye, Simba itakuwa imetulia tu na kikosi hikihiki!.

    Wako wapi akina Haruna Moshi Bobani, Kindoki hawa si ni kati ya wale aliowataka yeye na akafanikiwa kuwasajili, sasa mbona wamekalia benchi juzi! Sioni utetezi wake upo wapi hapo, ila ninachoona ni janja janja tu ya kutafuta unafuu mbele ya waajiri wake na washabiki wa Yanga.

    ReplyDelete
  5. Anakoelekea huyu kongo man ataikana hii timu kuwa yeye sio kocha wao na kwamba hawatambui

    ReplyDelete
  6. Hela ya kuingia makundi confederation cup mwaka jana waliipeleka wapi..unajua mimi sielewi Yanga shida ya hela inatoka wapi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic