February 17, 2019



KIUNGO mkabaji wa timu ya Yanga, Feisal Abdallah 'Feitoto' amesema kuwa hawana hofu na kupoteza mchezo wao wa jana mbele ya Simba, pia kuhusu viporo walivyonavyo Simba haviwapi presha.

Yanga jana wakiwa nyumbani walipoteza mchezo wao mbele ya Simba ikiwa ni mchezo wao wa marudiano baada ya ule wa mwanzo kumalizika kwa suluhu.

"Matokeo ya mpira ni ya aina tatu kuna kufunga, kufungwa na kushinda hivyo hakuna namna kile ambacho tumepata tunashukuru na bado mapambano yanaendelea.

"Niwapongeze wapinzani wetu wa Simba kwa kupata ushindi mbele yetu, hatuna hofu na viporo vyao hata kama watashinda vyote nasi tuna mechi mkononi tutafanya vizuri," amesema.

Licha ya kufungwa bado Yanga wanaendelea kushika nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 58 wakiwa wamecheza michezo 24 huku Simba wakiwa na pointi 39 twakiwa wamecheza michezo 16 tofauti ya michezo nane kuwa sawa na Yanga.

3 COMMENTS:

  1. Amekua ukitumia vibaya neno "wametoa tamko" kwa kweli matumizi yake sii hayo, mchezaji hawezi kutoa tamko la timu, tamko Ni official statement kwa lugha nyingine na hutolewa na uongozi, na si kila mtu katoa tamko Mara kesho katoa tamjo, naomba chukua kamusi ulielewe vizuri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic