February 17, 2019



MASHINDANO ya Taifa ya mbio za nyika yaliyodhaminiwa na DSTV pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika Moshi mwishoni mwa wiki hii yamezalisha timu ya Taifa itakayowakilisha taifa kwenye mashindano ya mbio ya dunia yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi Machi nchini Denmark.


Katibu Mkuu wa shirikisho la riadha Tanzania, Wilhelm Godabuday amesema mashindano ya mwaka huu yamekuwa na ufanisi mkubwa kwani yameshirikisha wanariadha wengi na pia kumekuwa na wanariadha wapya ambao wameonyesha uwezo mkubwa.

Timu hiyo ya taifa inajumuisha jumla ya wachezaji 28 katika Makundi manne ambapo kundi la kwanza ni wanaume wa umri wa zaidi ya miaka 18, la pili ni wanawake umri zaidi ya miaka 18, la tatu ni wavulana chini ya miaka 18 na la nne ni wasichana chini ya miaka 18.

Wachezaji watakaokua katika kundi la wanaume weneye umri wa zaidi ya miaka 18 ni Faraja Damas (Arusha), Joseph Panga (Arusha), Sylvester Marco (Arusha), Stephano Huche (Arusha), Deogratius Nade (Manyara), Yohane Elisante (Arusha) na Bazil Sule (Polisi)

Kwa upande wa wanawake katika kundi hilo ni Failuna Abdi (Arusha), Magdalena Shauri (JKT)Anjelina Daniel (Arusha), Amina Mohamed (Arusha), Marselina Issa (Arusha) na Neema Msuad (Arusha).

Kundi la wavulana chini ya miaka 18 litakuwa na wachezaji saba ambao ni Michael Kishimba (Arusha), Daniel Sinda (Arusha) Emmanuel Joseph (Manyara) Francis Damiano (Mbulu), Saimon Francis (Arusha) na Nicodemo Joseph (Mbulu) wakati wasichana watakuwa ni Agnes Protus (Arusha), Anastazia Ndoromongo (Arusha) Aisha Luguna (Arusha) Sara Hiti (JKT) Gace Jackson (JKT) Noela Lemmy (Arusha na Catherine Philipo (Manyara).

Kambi hiyo itakuwa chini ya jopo la wataalamu nane wakiongozwa na Kocha wa riadha Meta Petro kutoka Klabu ya Riadha ya Rift Valley. wengine ni Anthony Mwingereza (JWTZ), Anrea Panga (JKT), Thomas Tlanka (Arusha) na Juma Jambau (Singida).

 Mwanariadha maarufu mstaafu Marcelina Gwandu ameteuliwa kuwa muangalizi (Matron) wa Kambi hiyo huku Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dr. Hamad Ndee akipewa jukumu la kuratibu mafunzo hayo.

 Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania (DStv) Johnson Mshana, amesema kuwa DStv imekuwa ikishiriki kwa muda mrefu sasa katika kuinua mchezo wa riadha hapa nchini na kwamba ushiriki wao katika kufanikisha mashindano hayo ni katika mkakati wake endelevu wa kuhakikisha kuwa vipaji vya wanariadha vinakuzwa.

“Tuna mkakati kabambe wa ‘Ni Zamu Yetu’ ambao lengo lake kubwa ni kuhakikisha kuwa wimbo wetu wa taifa unapigwa katika michuano ya Olympic – hii ikimaanisha kuhakikisha kuwa nchi yetu inapata medali katika mashindano hayo makubwa," amesema.

Timu hiyo ya taifa itaweka kambi jijini Arusha kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya dunia kambi ambayo inafadhiliwa na DStv na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic