February 12, 2019


MBUNGE wa Jimbo la Iramba, na Raisi wa timu ya Singida United, Dr Mwigulu Nchemba, amewataka wale wa Yanga, Singida, Azam na timu zote kiujumla wenye tabia ya kuwashabikia wapinzani kuacha kufanya hivyo hasa kwenye mashindano ya kimataifa.

Simba leo itakuwa uwanja wa Taifa ikicheza mchezo wa marudiano hatua ya makundi, Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Nchemba amesema kuwa kwenye mashindano yote ya kimataifa huwa anaweka kando ushabiki na kutanguliza uzalendo mbele kwa manufaa ya Taifa.

" Simba ikifanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa itapata fursa ya kufungua milango kwa mafanikio, nchi yetu itaongezewa nafasi kama itafanikiwa kufika nusu fainaili itaongeza nafasi nne kama ambavyo Zesco ilifanya.

"Sasa kama ikifanya vizuri kwenye mashindano haya na kutinga hatua ya nusu fainali nafasi nne hawatashiriki wao wenyewe bali Yanga watakwenda, Azam FC watakwenda, Singida United watakwenda na timu nyngine, hivyo tunapaswa tuipe sapoti mashabiki wote," amesema.

3 COMMENTS:

  1. hiyo hela ya kiingilio si bora niongezee kwenye mchango wangu wa kila mwezi kwa timu ya yanga badala ya kwenda kuwanufaisha hao wapuuzi........kwanza nani anataka kwenda kushuhudia aibu nyingine tena.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaongez kwani tumekushika mkomo

      Delete
    2. HAHAHAHAHAHA kwa kweli asiyejitambua usimwelekeze kujitambua et nae ni shabiki duuuuuu hongera kijana endelea kuipa yanga sapoti kwa elfu mbili tu yanga itayashinda haya aliyonayo kwelimmmmmmm

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic