KOCHA mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa ili Simba ifanikiwe kushinda kwenye michezo yake ya kimataifa ni lazima kocha wa Simba, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji afumue upya kikosi chake cha ushindani.
Simba inawakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa ikiwa inashiriki kombe la Mataifa ya Afrika hatua ya makundi imekuwa na matokeo mabovu kwenye mechi zake za hivi karibuni baada ya kupoteza mechi mbili kwa kufungwa mabao 10.
Zahera amesema kuwa ukubwa na uwezo wa wachezaji wa Simba sio wa kubeza ila kinachowakwamisha ni mfumo ambao unatumika ndani ya kikosi pamoja na wachezaji kushindwa kutofautisha aina ya mashindano.
"Mfumo ambao unatumika na kocha sio ule wa ushindani na unaoweza kuleta matokeo hasa ukizingatia kikosi chake kimepoteza michezo yake miwili kwa idadi ya mabao mengi, sasa kama anahitaji kushinda ni lazima afanyie kazi hilo la mfumo kwanza mengine yatafuata.
"Nimeona anapenda kutumia 4:4:2 huu ni mfumo ambao unawapa taabu wenyewe bila kujua, pia kingine ni uelewa wa wachezaji wanacheza kama michezo ya kirafiki hakuna ushirikiano ndani ya timu kama uongozi na kocha hatakaa na wachezaji wake tutashuhudia mengi," amesema Zahera.
Mchezo unaofuata wa Simba ambao wapo kundi D ni dhidi ya vinara Al Ahly ambao utakuwa ni wa marudio utapigwa Februari 12 Uwanja wa Taifa.
hilo lipo wazi mwl anaelemewa na mfumo wake
ReplyDeleteKweli mwalimu abadilishe mfumo
ReplyDeleteHizi mbinu Zahera ajaribu kuzitumia yeye kwenye ligi huenda nae zitamsaidia
ReplyDeleteYake yanamshinda huyo
ReplyDeleteZahera akatumie hizo mbinu kwake...tangua aache kuchezea mechi Dar amekuwa anayumba yumba.kwa mini asitumie mbinu hizo?
ReplyDeleteMkuu kubali tu ukweli kuwa pale #Simba kwa sasa hakuna kocha..
DeleteLabda huyo msaidizi anaweza saidia mengi..!!
Sawa na swala kumpa simba mbinu ya kukamata wanyama porini.Hii ni ajabu ya kwanza kwa mwaka 2019!!!!!
ReplyDelete