February 8, 2019


BEKI wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amefunguka kuwa sababu kubwa ya Simba kupokea kipigo kizito nchini Misri imetokana na kuwa na beki nyepesi kupitika ‘chochoro’ pamoja na kushindwa kuwaheshimu wapinzani wao.

Cannavaro ambaye kwa sasa ni meneja wa Yanga, ameyasema hayo kufuatia Simba kupoteza mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri kwa kipigo cha mabao 5-0, wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Borg EL Arabi nchini humo.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Cannavaro alisema sababu kubwa Simba kupokea kipigo hicho kizito ni kutokana na kushindwa kucheza kwa malengo huku beki yao ikionekana kuwa nyepesi kupitika.

“Kilichotokea kwa Simba ni kama walikitaka wenyewe kwa sababu kwanza hawakutaka kuwaheshimu wapinzani wao lakini walisahau kwamba Al Ahly ni bora maana ukiangalia walicheza bila ya kuwa na malengo yoyote ndiyo maana wakapokea kipigo.

“Unapocheza na timu bora kwanza lazima uwe na mpango wa kwanza na wa pili lakini Simba hawakuwa nayo, pia walikosa wachezaji wa kuamua matokeo na kujitolea maana hata ukiangalia beki yao ilikuwa nyepesi kupitika na kuruhusu bao tano kwenye kipindi cha kwanza. Nafasi bado wanayo iwapo wakijipanga vizuri,” alisema Cannavaro.

1 COMMENTS:

  1. Itajulikana Siku mtakutana na uchochoro huo...nendeni mmpigie magoti kakolanya haraka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic