ZAHERA AJA NA MKWARA MWINGINE KWA SIMBA
KOCHA Mkuu wa Yanga Mkongoman, Mwinyi Zahera amesema kuwa wala hawahofii washambuliaji wa Simba kwani tayari ameweka mikakati ya jinsi ya kuwazuia huku akiapa kamwe hawatafurukuta watakapokutana.
Kauli hiyo, aliitoa hivi karibuni baada ya kumaliza mazoezi ya mwisho ya timu hiyo kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara watakaovaana na Simba, kesho Jumamosi.
Safu ya ushambuliaji ya Simba inaongozwa na Mganda, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere, John Bocco na Adam Salamba. Akizungumza na Championi Ijumaa, Zahera alisema kuwa alitumia siku mbili kwa ajili ya kuifanyia safu yake ya ulinzi itakayoongozwa na mkongwe, Kelvin Yondani, Andrew Vicent ‘Dante’ na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.
Zahera alisema, tangu wamefika Morogoro kwa ajili ya kuweka kambi, akili na nguvu nyingi alizielekeza kwenye safu ya ulinzi kwa kuwapa program maalum ya jinsi ya kuokoa na kuzuia hatari golini kwao kwa muda wa siku mbili kwa maana ya Jumanne na Jumatano.
Aliongeza kuwa, katika mchezo huo anataka kuona mabeki wake hawawapi washambuliaji nafasi ya kufunga bao golini kwao, hivyo tayari amewapa majukumu mabeki hao wa kati na wa pembeni ambao ni Paul Godfrey ‘Boxer’ na Gadiel Michael.
“Ninafahamu Simba wazuri mbele pekee, lakini nyuma kwao wabovu, hivyo tangu tumefika hapa Morogoro nilikuwa na program ya siku mbili kwa wachezaji wangu.
“Program hiyo ya siku mbili niliilelekeza kwa mabeki wangu, Yondani, Dante, Ninja na mabeki wangu wa pembeni Boxer na Gadiel na nilianza na mabeki kwa lengo la kuzuia mashambulizi na kuokoa hatari zote golini.
“Nashukuru katika hilo nilifanikiwa kwa kiwango kikubwa, w a c h e z a j i wangu walishika maelekezo yangu niliyokuwa ninawapa, hivyo sina hofu mashabiki wa Yanga wajiandae kushangilia ushindi,” alisema Zahera.
Nyundo inamhusu
ReplyDelete