KIKOSI CHA SIMBA KILICHOPEWA NAFASI YA KUIUA YANGA LEO HIKI HAPA
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, leo Jumamosi anaweza kuwashangaza wengi kwa namna ambavyo atapanga kikosi chake cha kwanza kuna uwezekano mshambuliaji tegemeo timu hiyo, Emmanuel Okwi, akianzia benchi.
Sapraizi hiyo anaweza kuifanya Aussems kutokana na aina ya mazoezi ya mwisho aliyowapa wachezaji wake jana Ijumaa kwenye Uwanja wa Boko uliopo Ununio, Dar.
Imezoeleka kuwa, Okwi anapokuwa fiti, huwa anaanza kikosi cha kwanza hasa kwenye mechi nyingi ngumu, lakini leo Jumamosi kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambao Yanga ni wenyeji, Okwi anaweza kuanzia benchi akiwaacha John Bocco na Meddie Kagere wakianza.
Championi ambalo jana lilikuwepo mazoezini hapo, lilimshuhudia Okwi akifanyishwa mazoezi maalum peke yake kwa kunyonga baiskeli maalum ya mazoezi huku wenzake wakiendelea na mazoezi ya pamoja.
Hata lilipofika zoezi la kufunga mabao, Okwi aliendelea na zoezi lake hilo hali ambayo inaonyesha dhahiri ana hatihati kuanza kikosi cha kwanza. Wakati Okwi akiwa na hatihati hiyo, beki kisiki, Juuko Murshid, jana alifanya mazoezi huku kwenye ugoko wake kukiwa na kifaa maalum cha kuzuia asijitoneshe jeraha lake la ugoko.
Juuko aliyetajwa kuwa kwenye hatihati ya kucheza mechi ya leo, jana alifanya mazoezi ya pamoja na wenzake huku kocha akimpanga kwenye safu ya ulinzi sambamba na Pascal Wawa akiwafundisha namna ya kuwazuia wapinzani. Akizungumzia mazoezi hayo ya mwisho kuelekea mechi ya leo, Aussems alisema: “Tumemaliza salama mazoezi, kilichobaki ni kusubiri wakati ufike, mechi ichezwe.
“Katika mchezo huu, kikosi changu kitakuwa na mabadiliko kidogo kutokana na masuala ya kiufundi ambayo siwezi kuyasema kwa sasa.”
Licha ya Aussems kusema kutakuwa na mabadiliko kwenye kikosi chake cha leo, lakini kuna uwezekano mkubwa wa kikosi hicho kikawa hivi; Aishi Manula, Zana Coulibaly, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Pascal Wawa, James Kotei, Clatous Chama, Jonas Mkude, John Bocco, Meddie Kagere na Hassan Dilunga.
CHANZO: CHAMPIONI
Kimetimia
ReplyDeleteMechi ya Yanga ni muhimu kwa Simba ni mechi ya kutafuta point tatu muhimu kupunguza ukubwa wa pengo la point kati yake na Yanga ili simba kuwathibitishia wapenzi na mashabiki wao kuwa wao kweli malengo yao ni kuutetea ubingwa wao na kupeleka maajabu kunako klabu bingwa Africa. Simba wakiifunga yanga basi watapata msamaha kutoka kwa mashabiki wao kwa uzembe walioufanya zidi ya Mashujaa na kunako kombe la mapinduzi,mashindano ya sport pesa na vipigo viwili vya aibu club Africa. kwa hivyo Simba kushinda mechi yao dhidi ya Ahly kamwe kusiwafanye wachezaji wa Simba kubweteka zidi ya Yanga kwani bado wana deni na kamwe kauli ya Mwenyekiti Mo haija futika yakwamba Simba haitokuwa tayari kuendelea na mchezaji asiipigania klabu ni bora hata kubakia na wachezaji wachache wenye kujitoa kwa ajili ya klabu na kuja kufanya mchakato mpya wa kutafuta wachezaji wapiganaji wapya kwa ajili ya klabu. Wachezaji wa Simba lazima waelewe wanaingia uwanjani leo kucheza na Yanga wakiwa wanatimiziwa mahitaji yao yote na marupurupu juu wakati wenzao wachezaji wa Yanga wanaingia uwanjani wakiwa na njaa,wengi wa wachezaji wao wanaingia uwanjani wakiwa hawajalipwa mishahara yao ya miezi kazaa na wachezaji wao wengine wangali wapo kunako migomo. Sasa katika hali hiyo ya Yanga kama watakwenda kuifunga Simba leo pale Tifa kwanini simba isitafute wachezaji wengine?
ReplyDeleteKwangu mimi hii ya dabi ya Simba na Yanga, viongozi na makocha wa Simba waichukulie kama mechi ya kuijenga na kuiandaa timu kwa ajili ya mechi ya ugenini zidi ya Js Saoura. Ni ngumu lakini wanatakiwa kuiandaa sasa kushinda mechi ya ugenini zidi ya Js Saoura ikiwezekana hata kwenda kuweka kambi fupi ya maandalizi Misri au Tunisia ili kuzowea mazingira ya masaa ya mechi kwani hali za hewa za nchi hizi zinafanana. Kwakuwa Simba walishamalizana na Ahly kambi fupi Misri kwa Simba kwa ajili ya Js Saoura nadhani ni sehemu sahihi. Kwanini Simba lazima washinde mechi yao ya ugenini zidi ya Js Saoura? Kwa sababu Alahly sio rahisi kukubali kupoteza michezo miwili mfululizo. Kuna uwezekano mkubwa wa Ahly kwenda kumpiga As vita kwao. Na kama hiyo ikitokea basi As Vita hata akija akishinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Simba ataishia point saba 7 na Simba akifanikwa kumpiga Js Saoura basi Saoura hata wakishinda mechi yao mwisho wataishia na point zao nane 8 na kumuacha simba na point zake tisa 9 .kwa maana hiyo mechi ya kuipeleka Simba robo fainali club ya Africa ni mechi yao dhidi Js Saoura ugenini na kufanya kosa kwa mtu au taasisi inayojitambua huwa ni moja ya njia ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo na baada ya Simba kuchezea vipigo viwili vya aibu ugenini nadhani iwe fundisho tosha la kwenda kusahihisha makosa Algeria.Mechi ya Simba na Js Saoura ugenini wadau wa mpira nchini wasisubiri kuja kulaumu na kuicheka Simba bali tuichukulie kama jukumu la taifa yaani piga ua hiyo mechi Simba lazima ashinde na inawezekana na hata kama haitawezekana basi tutakuja kujifunza na jitihada zetu tulikosea wapi ili lijekuwa fundisho la baadae, and yes we can mimi ni muumini wa kuamini kunako jitihada hakuna lisilowezekana na kukata tamaa kwa mtu juu ya uwezo wa kufanikisha jambo ni dalili za kumdhrau Mungu na laana yake siku zote ni kubwa na ndio maana watanzania tunabakia kuwa masikini na omba omba wakati hatuna kasoro yoyote ya maumble na hata kama tungekuwa na kasoro ya maumble ya viungo kama akili nzima basi bado tunauwezo wa kufanya makubwa.