BANKA YAMKUTA TENA YANGA, ATUPWA NJE
KIUNGO mchezeshaji wa Yanga, Issa Mohamed ‘Mo Banka’ yamemkuta tena kwenye timu hiyo baada ya enka yake kuvimba kwenye mguu wake wa kushoto.
Banka amepata majeraha hayo ikiwa ni siku chache tangu arejee kuichezea timu hiyo kwenye kikosi cha Mkongomani, Mwinyi Zahera baada ya kutoka kifungoni.
Kiungo huyo, alikutana na adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja na Fifa baada ya kukatana na skendo ya kutumia madawa wakiwa kwenye michuano ya Chalenji iliyofanyika nchini Kenya akiwa anaichezea timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes.
Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema kuwa kiungo huyo amepewa mapumziko maalum huku akiendelea na matibabu baada ya enka yake kuvimba.
Saleh alisema, kiungo huyo ameondolewa kwenye mipango ya kocha msaidizi wa timu hiyo Mzambia, Noel Mwandila kwa ajili ya kumtumia katika mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Alliance United utakaopigwa Machi 30, mwaka huu.
“Banka ameondolewa katika mipango yetu ya mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho kutokana na uvimbe mkubwa uliokuwepo katika enka aliyoipata akiwa mazoezini.
“Tofauti na Banka, mchezaji mwingine atakayeukosa mchezo ni Mwinyi, Abdul wote wana malaria, Dante maumivu ya misuli na Ninja anayetumikia kifungo cha michezo mitatu,” alisema Saleh.
Pole kijana,ukipona utaendelea na majukumu yako
ReplyDelete