March 23, 2019


Msanii mkongwe wa filamu nchini, Mzee Hashim Kambi, amedai kua kitendo cha waandaaji wa Tuzo za Sinema Zetu International Festivals (SZIFF) kuwapa tuzo ya Waigizaji Bora, watoto Flora na Rashid, hakikuwa cha kiungwana kwani katika hali ya kawaida tu ni ngumu watoto hao kuwashinda waigizaji wakubwa kama vile Gabo, Wema, Johari.

Mzee Kambi amesema watoto hao walipaswa kupewa tuzo ya wasanii bora chipukizi na si kuwapa tuzo ya waigizaji bora kutokana na umri wao, lakini hata kama ni kuhesabu kura walizopigiwa na mashabiki basi hawana umaarufu wala uwezo wa kuwashinda wakina Wema na Gabo.

Aidha, Mzee Kambi ameongeza kuwa hapendezwi na kitendo kinachofanywa na Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, cha kuisifia Simba mara zote anazoitwa katika tuzo hizo kwa ajili ya kumkabidhi mshindi tuzo yake.

2 COMMENTS:

  1. Anachokereka nini? Manara ndio kazi yake.Yeye huyu mzee uyanga inamsumbua.Na yeye si aisifie Yanga nani kamkataza.Aache kuingilia uhuru wa watu.

    ReplyDelete
  2. duh! hadi kwenye jukwaa la uigizaji anaisifu simba yake!!!? ndo robo ishamlevya ndg yetu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic