March 7, 2019


OBREY Chirwa amewaambia washikaji zake pale Yanga kwamba anatamani kurudi Jangwani ingawa Azam wanamlipa mkwanja mzuri.

Mzambia huyo alikuwa Yanga akatimkia Misri kwa madai kwamba njaa ilizidi lakini Hans Pluijm akamvuta Azam akamwaga wino. Pluijm amepigwa chini akamuacha Chirwa Azam.

Kwa mujibu wa Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, Chirwa amemuendea hewani besti mmoja ambaye ni mchezaji wa kikosi cha kwanza akamwambia anatamani kurudi Yanga.

“Unaona yule Chirwa anayecheza Azam, kule kuna kila kitu lakini amempigia simu mchezaji wangu mmoja ambaye ni rafiki yake akamwambia anatamani kurudi Yanga,” alisema Zahera alipotembelea Ofisi za Global Publishers Sinza Mori, Jijini Dar es Salaam, juzi Jumanne na kuongeza.

“Pale Azam kuna kila kitu lakini mchezaji kama Chirwa alishakuwa na mtandao wa watu wengi, alikuwa ana uwezo wa kufanya mambo yake bila kutegemea mshahara.

“Lakini ilifi ka mahali akajisahau akaondoka Yanga, sasa hivi anawaambia wenzake kwamba pale Azam anaishi kwa kutegemea mshahara tu hakuna zile pesa za pembeni na watu wa Yanga hawawezi kumpa sasa hivi kwavile siyo mchezaji wao.

“Ndio maana niliwaambia wachezaji wangu Yanga hakuna mshahara tuko kwenye hali mbaya, lakini tukishinda tutapata pesa nyingi kuliko mishahara.

“Na kweli kila tukishinda wachezaji wanapata zaidi ya laki mbili, hizi gharama kama za kodi ya nyumba, kulipia luku ni mambo ambayo wanazipata kwa mashabiki wakishinda.” Zahera alisisitiza kuwa kutokana na hela hizo wanazopata wachezaji wake kutoka kwa wadau, ndizo zinawafanya kuzidi kuwa na mzuka.

CHANZO: SPOTI XTRA

3 COMMENTS:

  1. “Unaona yule Chirwa anayecheza Azam, kule kuna kila kitu lakini amempigia simu mchezaji wangu mmoja ambaye ni rafiki yake akamwambia anatamani kurudi Yanga"
    HAYA BANA...Ila Zahera anapaswa kujua kuwa watanzania sio wajinga!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Zahera haoni kama anamjengea chirwa mazingira ya kutocheza vizuri dhidi ya Yanga.nadhanni kwa level yake hapaswi kuzungumzia sanna hisia za wachezaji wa timu nyyingine.ni kuwatoa mchezoni.v

      Delete
  2. Anaanza kuwaharibu wachezaji kisaikorojia, kwa Chilwa, Zahera anajua wana mechi na Azam inakaribia, na anafahamu kuwa Chilwa ni mwiba kwa kikosi cha Azam kikikutana na Yanga, hawatamuweza. Sasa anaanza kutengeneza mazingira ya kumharibu mchezaji kisaikorojia pia kuwafanya waajiri wake (Chilwa), yaani Azam FC Washindwe kumuamini pindi ikifika mechi baina yao na Yanga.

    Ushauri wangu ni kwamba; Binafsi naomba TFF isimame wima na kuchukua hatua kwa watu kama Zahera ambao wanaongea hadi wanavuka mipaka. Kama yeye ameshakuwa Msemaji wa timu ya Yanga, itoshe kuzungumzia habari zao za Yanga tu, na sio kuingilia masuala na wachezaji wa timu zingine. Hizo mbinu zake za Watawala wa Kifaransa Tanzania hatuzitaki.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic