March 15, 2019


WAPINZANI wa Simba kwenye mchezo wa kesho wa Ligi Mabingwa jana walianza kupiga mazoezi kujiaandaa kuwawinda Simba kwenye Viwanja vya Gymkhana.

AS Vita waligoma kuzungumza chochote jana wakati wa mazoezi ambapo wanajua kwamba kesho muziki utakuwa mzito kutokana na kundi D kila mmoja kuwa na falsafa ya kushinda nyumbani.

Simba wana kazi kubwa kutafuta matokeo kesho ili kupenya hatua ya robo fainali ambapo kwa sasa kundi lao limekaa kimtegomtego.

Simba ambao wapo nafasi ya nne wana pointi sita wakishinda mchezo wa kesho wanatinga hatua ya robo fainali wakitoa sare ama kupigwa ndio mwisho wa safari yao.

Al Ahly wao wana pointi saba watamenyana na JS Saoura wenye pointi nane, hapa hesabu tu, Al Ahly ana hitaji ushindi wa aina yoyote kama atapata sare ndo mwisho wa safari JS Saoura anapenya.

Leo AS Vita watafanya mazoezi Uwanja wa Taifa ikiwa ni maandalizi ya mwisho kabla ya kesho kuivaa Simba, mchezo wa kwanza nchini Congo walishinda mabao 5-0.

Uongozi wa Simba umepania kupindua meza kibabe ambapo nao leo pia watafanya mazoezi Uwanja wa Taifa.

2 COMMENTS:

  1. Once again a great posts by you
    please tell me how we can make money via forum posting?
    I’m using forum posting to get some extra traffic to my blog via signature links but never think to make money from it ??
    Hope to get more knowledge from you.
    Regards!
    just click here Visit my Site goodnewsagency24"

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic