March 15, 2019

KOCHA Mkuu wa JKT Tanzania, Bakari Shime amesema kuwa kwa sasa hana cha kufanya kutokana na mabosi zake kufikia uamuzi wa kumsimamisha kazi bila kuogea naye alichokosea.

Uongozi wa JKT Tanzania uliamua kumsimamisha Shime kwa kile walichoeleza kutoridhishwa na mwenendo wa kikosi chake kwenye ligi.

"Sina cha kufanya kwa sasa kwa sababu naheshimu mkataba wangu, nasubiri niitwe kusikiliza maamuzi na madai yao kuhusu mimi ila bado sijajua hatma yangu kwa kuwa sijaambiwa lolote zaidi ya kuskia kwenye vyombo vya habari, ila kuna timu ambazo zimeanza kunifuatilia," amesema Shime.

JKT Tanzania kwa sasa ipo nafasi ya 9 baada ya kucheza michezo 30 ikiwa imejikusanyia pointi 36, mchezo wake wa mwisho ilifungwa mabao 6-1 dhidi ya Azam FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic