KESHO Yanga itakuwa kazini kumenyana na Lipuli, Uwanja wa Samora ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Wachezaji wanne watakosa mchezo huo wa kesho kwa mujibu wa kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera hawa hapa:-
Abdalah Shaibu 'Ninja', Andrew Vincent 'Dante', Juma Abdul na Ibrahimu Ajibu ambaye ni nahodha wa timu kwa sasa.
Zahera amesema kwa mujibu wa daktari wa Yanga, Edward Bavu kuwa Ajibu ni majeruhi, Ninja ana adhabu anaitumikia, Dante na Abdul bado ni wagonjwa.
Yanga imejikita kileleni ikiwa na pointi 67 kwa sasa baada ya kucheza michezo 27.
0 COMMENTS:
Post a Comment