March 15, 2019


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema hana nia mbaya kuwa karibu na timu ya AS Vita kama ambavyo Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amekuwa anadai.

Zahera ameeleza uwepo wake wa karibu na Vita ni kwa sababu timu hiyo ina wachezaji takribani watano wanaoichezea timu ya taifa ya Congo.

Kocha amesema asitafsiriwe vibaya kwani wale ni sawa na ndugu zake na muda mwingi anakuwa haonani nao kutokana na kubanwa na majukumu ya kazi.

Kutokana na sintofahamu juu yake, Zahera amemtaka Manara asianze kumlaumu kwani hawezi kufanya lolote baya kuelekea mechi yao ya kesho na Vita kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Unajua ile timu ina wachezaji takribani watano wanacheza timu ya taifa, ninawafundisha, sina ubaya wowote na yale anayoyasema Manara.

"Asinitafsiri vibaya kwani si vibaya kwenda kusalimiana nao maana ni ndugu zangu, ni wakongo wenzangu.

CHANZO: EFM

7 COMMENTS:

  1. Kawasilimie Wakongo wenzako lakini kesho ni kipigo kikubwa



    ReplyDelete
  2. Yaonekna anajihami. Ajui kama wewe ni mkongo aache uwoga

    ReplyDelete
  3. Manara kwel hamnazo,sasa zahera asipokuwaa karibu na Vita club awe karibu na NanπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

    ReplyDelete
  4. Mwambie aende na Leo asubuhi kuwajulia hali awaulize na matokeo

    ReplyDelete
  5. Wendawazim wa yanga aushi anaachaje tim yake inaenda kwa lipuli yeye abaki hapa na as vita sasa kikowapi

    ReplyDelete
  6. Zahara chiz atawaacha kwenye mataa cku mkikutana na tp mazembe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic