March 2, 2019

MABINGWA watetezi Simba ambao wanaparamia viporo vyao kwa sifa, kesho wanaingia kwenye anga nyingine za Stand United kwenye mchezo wao utakaochezwa Uwanja wa Kambarage.

Simba wanaingia Uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kuwatandika mabao 3-1 wapinzani wao wa muda wote Lipuli ambao walishindwa kuwafunga walipokutana nao mara tatu, huku Stand United nao wanaingia wakiwa wanakumbukumbu ya kuwanyoosha haohao Lipuli kwenye Uwanja wao wa Kambarage mabao 3-2.

Kinara wa mabao kwa Simba, Meddie Kagere amesema anatambua ushindani uliopo ila heshima tu itawabeba wafanye poa kwenye mchezo wao wa kesho.

"Hakuna timu nyepesi, baada ya mchezo mmoja kuisha kinachofuata ni maandalizi ya mchezo wetu unaofuata hatuna presha tunapambana kwa ajili ya timu na mashabiki, kikubwa sapoti," amesema Kagere mwenye mabao 12 kwenye ligi kwa sasa.

Simba inacheza kesho mchezo wake wa 20 ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 48 ambazo zinaifanya ijiwekee utawala wake kwa muda nafasi ya tatu kwa sasa kwenye msimamo wa ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic