March 17, 2019


Benchi la ufundi la AS Vita jana liligoma wachezaji wao wasiingie kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwa sababu wanahofia kuwa na sumu.

Mmoja wa viongozi wa benchi hilo aliyejitambulisha kwa jina la Daktari Noar alisema, walikuwa na  uhakika chumba walichoandaliwa kwa ajili ya mapumziko na kubadilishia nguo kuna dawa ambazo ni kwa ajili ya kiwaumiza wachezaji wao.

Wachezaji AS Vita ambao waliingia na kukaa kwenye korido walionekana wakiwa wamevalia viziba pua na mdomo vyeupe.

“Tuna uhakika chumba hiki kimepulizwa sumu lakini kwa sababu hatuna vipimo ni ngumu kugundua ni aina gani,”alisema Noar.

Alisema tukio kama hilo kufanyika kwao si mara ya kwanza ilishawatokea katika nchi moja kusini. Amesema, yote hayo ni mbinu za mchezo. Kocha wa AS Vita alibaki anaguna na kunungunika.

1 COMMENTS:

  1. Na ile kitendo cha kujisaidia haja ndogo ktk koriddor vipi???

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic