March 14, 2019


UNAVYOSOMA hapa muda huu, Yanga iko njiani inaitafuta Iringa kwenda kuivaa Lipuli FC huku ikiwakosa nyota wake Vicent Andrew ‘Dante’ na Juma Abdul huku Abdallah Shaibu akitumikia adhabu. 

Yanga Jumamosi itavaana na Lipuli FC katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa huku msimu uliopita Yan¬ga iliweza kushinda kwa mabao 2-0. 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mratibu wa Yanga, Hafidhi Saleh alisema ; “Kule hatutaenda na Dante na Juma Abdul ambao wote ni wagonjwa na Ninja yeye inajulikana kama ana adhabu ya mechi tatu ni hao tu wengine wote wako .” 

“Lipuli sio timu mbaya ila na sisi tunaji¬panga kuona timu yetu inaendelea kupata matokeo mazuri ilikuwa kwenye nafasi nzuri zaidi,”alisema Hafidhi.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic