March 14, 2019

 
MZEE Ibrahim Akilimali amewaambia mashabiki wa Yanga kwamba; “Niombeeni, kisukari kinanitesa sana.”
Mwenyekiti huyo wa Baraza la Wazee wa Yanga, jana hakuweza kuzungumza kwa kirefu na Spoti Xtra kwa maelezo kwamba hajisikii vizuri kabisa. 



Hivi karibuni Akilimali alilazwa maeneo ya Baobab katikati ya Bagamoyo na Bunju akisumbuliwa na ugonjwa huo wa kisukali uliomfanya awe kitandani na kuwa kimya kwa sasa. 


Akilimali amekuwa na mvutano mkubwa na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kwa madai kuwa ndiye aliyechangia kuondoka kwa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji. 


Akizungumza na Spoti Xtra ambalo linaongoza kwa mauzo kila Alhamisi na Jumapili, Akilimali alisema kuwa, kwa sasa hayupo vizuri kutokana na hali yake kuendelea kuwa tete ambapo yupo Bagamoyo akijiuguza maradhi yake hayo. 


“Hali yangu bado ipo hivyo hivyo sijatengemaa, sijisikii vizuri, nipo huku Bagamoyo nikijiuguza hata kuzungumza vizuri siwezi, uniwie radhi,” alisema Akilimali ambaye ni msomaji mzuri wa Spoti Xtra.

2 COMMENTS:

  1. Pole mzee wetu tumekumisi Sana utapona mungu akusaidie

    ReplyDelete
  2. مدونة شعاع معاً وبتعاون مع الجميع نطور العالم العربي
    فهي طريقك الاول لتوسيع نطاقك المعرفي في جميع المجالات
    مدونة شعاع
    المجتمع
    الأخبار
    الصحة
    الجمال
    الربح من الأنترنت
    روايات
    برامج
    العاب
    التاريخ
    للتواصل والعمل معاً واتساب +201027451442

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic