JPM AKUTANA NA TIMU YA WATAALAMU WA UJENZI WA UWANJA MKUBWA WA MPIRA DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya wataalamu wa Tanzania na Morocco wanaoshughulikia ujenzi wa uwanja wa michezo katika Jiji la Dodoma, unaotarajiwa kujengwa kwa msaada wa Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI
Balozi wa Morocco hapa nchini aliyeongoza ujumbe wa wataalamu kutoka Morocco Mh. Abdelilah Benryane, amesema pamoja na kuzungumzia uhusiano mzuri wa Tanzania na Morocco wamejadiliana kuhusu utekelezaji wa miradi iliyokubaliwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco hapa nchini mwaka 2016.
Ukiachana na Uwanja, moja ya suala lingine ambalo litatekelezwa ni ujenzi wa Msikiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale amesema uwanja huo utajengwa jirani na eneo la Nanenane kando ya barabara ya Dodoma – Morogoro, utajengwa kwa mfano wa mlima Kilimanjaro na utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji kati ya 85,000 na 100,005.
0 COMMENTS:
Post a Comment