March 13, 2019

BARAZA la wadhamini wa klabu ya Yanga, chini ya Mwenyekiti wake, George Mkuchika limependekeza klabu hiyo kufanya uchaguzi wake mkuu mwaka huu 2019 badala ya mwaka 2020.

Mkuchika amesema kuwa mapendekezo hayo yatapitishwa na wanachama wa Yanga kupitia mkutano mkuu ambao wataitisha hivi karibuni.

"Tunatarajia kufanya uchaguzi wa nafasi zote mwaka huu na ili hilo liweze kufanyika tutaita mkutano kwa wanachama wote ili kujadiliana isije ikawa wakasema tunaburuzana.

"Mkutano mkuu wa uchaguzi wa Yanga mwaka huu tutaufanya hivi karibuni ili kupeleka maoni haya kawo nao  wakikubali mchakato huu ufanyike na itakuwa ni kuanzia  sasa tutafanya huo mkutano ndani ya wiki mbili au tatu hivi," amesema Mkuchika.

Yanga haijafanya uchaguzi wa kuchagua viongozi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wao Yusuf Manji kujiuzulu na imekuwa ikiripotiwa atarejea ila bado hajarudi mpaka sasa.

4 COMMENTS:

  1. Migongo wazi kwa kudanganyana .Kwani Leo ndio wamejua kwamba kuna uchaguzi wa Nchi mwaka kesho.
    Tutaanza kusikia tena Manji atarudi nä wapo wataopiga magoti.
    Ujinga ni maradhi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mikia FC fieni mbali huko! Mnasubiri asante ya MO Dewji ngojeni club ainunue Eti!

      Delete
  2. Yanga kuweni makini na maamuzi yenu ya kuhairishahairisha uchaguzi na kutoa mianya ya kuleta sintofahamu fanyeni hiyo mikutano yenu haraka na muwasihi wanachama kuacha kukimbilia mahakamani kufungua kesi na kuleta mshikamano na umoja haraka sasa uchaguzi ufanyike mwezi 4 mkutano mkuu wa wanachama ufanyike mwisho wa mwezi 3. Ili mchakato uende haraka na muwe na uongozi unaosimamia timu kwa ufanisi....muende kwenye mfumo wa uwekezaji kuanzia mwezi 6. Fanyeni haya haraka mko nyuma sana!!!!!...leteni wawekezaji kuunda kampuni ya michezo ya Yanga kuanzia juni Mwekezaji aanze kutafutwa kuanzia mwezi 5....huo ni ushauri wangu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic