UONGOZI wa KMC umesema kuwa hawana hofu kuwakabili vinara wa Ligi Kuu Bara kwa sasa, Yanga katika mchezo wa leo utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
KMC wataingia Uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa kufungwa bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa mzunguko wa kwanza.
Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde, amesema kuwa wamejipanga kiasi cha kutosha kuona wanaibuka kidedea mbele ya wapinzani wao Yanga leo.
"Kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Yanga, mbinu ambazo wachezaji wamepewa na kocha Ettiene Ndayiragije zinatosha kuwamaliza wapinzani wetu na kutufanya tubebe pointi tatu.
"Tunatambua ushindani ni mkubwa hivyo nasi tutaleta ushindani ili tubebe pointi tatu hakuna namna nyingine itakayotufanya tuwe katika mazingira mazuri kwenye ligi kwa sasa zaidi ya ushindi, mashabiki wajitokeze kutupa sapoti," amesema Binde.
0 COMMENTS:
Post a Comment