KOCHA Mkuu wa timu ya JKT Tanzania, Bakari Shime 'Mchawi Mweusi' amesema kuwa mchezo wao wa juzi walicheza usiku hali ambayo ilileta changamoto kwao na kupokea kichapo cha mabao 6-1 dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Chamazi.
Akizungumza na SpotiXtra, Shime alisema kuwa kupoteza mchezo ni sehemu ya matokeo ila kufungwa mabao sita sio jambo la kawaida hasa kwa timu ambayo imejipanga kuleta ushindani ndani ya timu hivyo atakaa na wachezaji ili kutambua tatizo ambalo linawasumbua kwa sasa.
"Mchezo wetu tumecheza usiku hali ambayo kidogo ilikuwa na changamoto kwa wachezaji ila nimegundua mambo mengi na nimejifunza, kwa sasa natuliza akili, nitawakalisha chini wachezaji wangu kisha tujue namna bora iakayotusaidia kupata matokeo chanya.
"Ushidani ni mkubwa na kila timu inahitji matokeo, naamini bado tuna nafasi ya kufanya vizuri hasa ukizingatia tofauti kwenye timu za ligi kuu ukiachana na zile tatu ambazo ni Simba, Yanga na Azam ni ndogo, hesabu zetu bado zinatulinda," alisema Shime.
Mchezo unaofuata kwa JKT Tanzania ambayo imecheza michezo 30 ikiwa na pointi 38 ni dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Machi 15 Uwanja wa Sokoine.
0 COMMENTS:
Post a Comment