March 9, 2019


Na George Mganga

Shabiki maarufu wa timu ya Simba, Said Hamis maarufu kwa jina la Muchacho, amesema kukoseka kwa straika Mganda, Emmanuel Okwi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura leo hakutaonekana mapungufu.

Okwi amesalia nchini kutokana na hali yake kiafya kutoruhusu hivyo atakuwa anawatazama wenzake wakicheza usiku wa leo huko Algeria ukiwa ni mchezo wa mkondo wa pili timu hizo kukutana.

Muchacho ameeleza kukosekana kwa Okwi hakutaonekana pengo lolote lile kwani anamuani Meddie Kagere kuziba nafasi yake.

Mbali na Kagere, Muchacho amemtaja pia John Bocco kuongeza makali kwenye safu hiyo ambaye amekuwa pia sehemu ya kikosi kilichosafiri kuwakabili Saoura.

"Hakutakuwa na pengo lolote lile, Kagere yupo na lazima atawaonesha kazi Saoura. Bocco pia yupo kwahiyo hakuna tatizo lolote." amesema.

Simba inaenda kucheza na Saoura ikiwa na kumbukumbu ya ushindi kwenye mechi ya awali iliyochezwa Dar es Salaam kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic