KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema kesho moto utawaka Samora mbele ya wapinzani wao Mbao FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Matola amekuwa katika wakati mgumu kwa sasa kupata matokeo kutokana na ukata ambao unakisumbua kikosi chake kwani ilielezwa kuwa wachezaji wake waligoma kufanya mazoezi kushinikiza walipwe mishahara yao wanayodai.
Matola amesema ugumu wa uendeshaji kwa timu unatokana na wadau wengi kushindwa kumudu gharama, kwani hali imekuwa ngumu na kutokuwepo kwa mdhamini mkuu kwenye ligi kunachangia.
"Kesho natambua nitakuwa na mchezo mgumu ila hesabu zangu ni kuona namna gani naibuka na ushindi mbele ya wapinzani wangu Mbao.
"Naiheshimu timu pinzani kwani si ya kuibeza ila nimewaandaa wachezaji kupambana na kutafuta matokeo kwenye Uwanja wa nyumbani," amesema Matola.
Mshambuliaji wa Mbao, Said Junior amesema wapo tayari kupambana na kutafuta pointi tatu kwani wana hasira baada ya kupoteza mbele ya Mtibwa Sugar.
Jumla ya pointi tisa mpaka sasa Matola amepoteza mfululizo baada ya kuanza kupigwa na Stand United kikafuata kipigo cha Simba na hivi karibuni mbele ya Kagera Sugar.

0 COMMENTS:
Post a Comment