March 11, 2019


KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, imetangaza kumfungia mechi mbili pamoja na faini ya laki tano, kocha mkuu wa timu ya Alliance FC, Malae Hamsini kwa kosa la kuzozana na mashabiki.


Kwa mujibu wa Wambura, amesema Kamati hiyo imefikia maamuzi hayo baada ya kocha huyo kuzozana na mashabiki wakati wa mchezo dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Chamazi.

Katika mchezo huo amesema kuwa Hamsini alitoka kwenye benchi la ufundi na kuwafuata mashabiki wa timu ya Azam kuzozana nao jambo ambalo halikubaliki kisheria.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic