March 11, 2019


Watani wa Jadi Yanga na Simba wapigwa faini kwa makosa waliyoyafanya katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara, uliowakutanisha Februari 16 mwaka huu.

Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema kuwa kulikuwa na vitendo vya ajabu katika mchezo huo kitu ambacho kilipelekea kamati ya masaa 72 kukaa na kutoa maamuzi juu ya Vilabu hivyo.

Kwa upande wa Klabu ya Yanga imepigwa faini ya milioni 6 kwa kosa la kuingia Uwanjani kwa mlango usio rasmi pia kutoingia vyumbani na kusababisha wachezaji kukaguliwa wakiwa koridoni.

Klabu ya Simba pia imepigwa faini ya milioni 3 kwa kuingia Uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.

8 COMMENTS:

  1. hii kamati kazi yao ndio hiyo ya kunyan'ganya pesa kutoka kwenye vilabu na kujaza matumbo yao badala ya kuendeleza soka hata ligi ikiisha washavuna mabilioni ya shilingi na soka kila siku linadidimia.

    ReplyDelete
  2. Nikweli kaka wanafanya hivyolakini na timu zetu zimezidi mambo ya kishirikina nadhani wangekua wanawanyanganya point ili iwe fundisho

    ReplyDelete
  3. hizo pesa za adhabu matumizi yake yakoje??????????

    ReplyDelete
  4. Bodi ya ligi waoneeni huruma Yanga! Pesa yenyewe hadi kwa bakuli hiyo milioni 6 wataitoa wapi mwa jameni! Bora faini zote mngeipiga Simba Milionea

    ReplyDelete
  5. mlizipigia sana maesabu hizo pesa za bakuli... mkataka makato ya serikali ikashindikana sasa mmepata mwanya mmeona mpige mill sita kabisa!! duh.. na round ya kwanza mchezaji wa simba () alivyo mpiga ngumi mbili mchezaji wa yanga yenyewe ilikuwa fear game? mnazingua kabisaaa

    ReplyDelete
  6. Aise mtawatia masikini yongo yongo fc

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic