March 11, 2019


ALIYEKUWA Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ wameendelea kusota rumande baada ya kesi yao kuahirishwa hadi Machi 20, mwaka huu.

Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar chini ya wakili Simba, lakini iliahirishwa baada ya upande wa washitakiwa kuomba kuahirishwa kutokana na mawakili wao watetezi kutokuwepo.

Kwa upande wa Takukuru, wamemleta shahidi Prisca Daudi akitokea Benki ya CRDB Mikocheni ili aweze kutoa ushahidi, lakini kutokana na udhuru huo ameshindwa kufanya hivyo. Kufuatia maombi ya upande wa washitakiwa, Wakili Simba amekubali kuahirisha kesi hiyo hadi Machi 20, mwaka huu huku akitaka kesi hiyo imalizwe haraka kwa kuwa ni ya muda mrefu.

Alieleza kuwa lengo ni kuhitaji kuimaliza kesi hiyo mapema ikiwezekana ifikapo mwezi wa nne iwe imeshamalizika kwa kuwa watu wengi wanasubiria majibu ya kesi hiyo. Aveva na Kaburu wanakabiliwa na makosa takribani matano ikiwemo ya utakatishaji fedha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic