March 11, 2019


KOCHA anayepiga 'deiwaka' Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa kikubwa kilichomshinda kocha aliyefungashiwa vilango, Hans Pluijm na Juma Mwambusi ni kutoelewa tabia za wachezaji wa Azam.

Rekodi zinaonyesha kwamba ushindi wa mechi mbili za awali kwa Pluijm ilikuwa wa jumla ya mabao 5 rekodi ambayo imevunjwa na Cheche ambaye kwa michezo miwili ameshinda jumla ya mabao 9.

Cheche amesema kuwa kikubwa ambacho kwa sasa kinambeba kwenye kazi ni uzoefu alionao ndani ya Azam pamoja na kuzijua tabia za wachezaji wote wa kikosi chake.  

"Wakati wanaifundisha Azam, walimu walopita walikosa muda wa kukaa na timu na kutotambua ubora wa wachezaji hivyo hicho ndicho kilichokuwa kikiwashinda pamoja na namna ya kuwatumia.

"Tofauti ni kwamba sisi tunawatambua wachezaji wetu na tabia zao, hivyo haikuwa ngumu kwetu kuwatumia na tunaamini tutaendelea kupata matokeo mbele ya wapinzani wetu," amesema Cheche.

Mchezo ujao kwa Azam ambayo kwa sasa imejikita nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 27 ikiwa na pointi 56 utapigwa Uwanja wa Chamazi Machi 16.dhidi ya Singida United.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic