March 17, 2019


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa hawakuwa na chaguo jana zaidi ya kupata ushindi mbele ya wapinzani wao AS Vita kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Taifa.

Simba imetinga hatua ya robo fainali Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 jambo ambalo limewafurahisha mashabiki wa Simba na Taifa kiujumla.

Aussems amesema ilikuwa ngumu kwake kupoteza na hakufikiria kushindwa kutokana na nguvu ya kundi hasa kwa namna linavyopata matokeo kwenye michezo ya kimataifa.

"Ukiangalia namna ilivyokuwa kwa timu nyingi hasa kwenye kundi letu hatua ya makundi zilikuwa zinapata pointi nyumbani, sasa kama wao waliweza kwa nini iwe ngumu kwetu kushinda? Hivyo niliwaambia wachezaji hawana kazi mpya Uwanjani zaidi ya kushinda na ndicho kilichotokea.

"Mabao mengi tumefungwa ila sisi hatukuwa na presha hesabu ilikuwa ni pointi tatu, mashabiki wa Simba na Taifa kiujumla wamefanya jambo jema na tunajivunia kupenya hatua hii muhimu," amesema Aussems.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic