March 17, 2019


KIUNGO wa timu ya Yanga, Thaban Kamusoko amesema kuwa kilichowafanya jana kushindwa kupata matokeo mbele ya kikosi cha Lipuli, Uwanja wa Samora ni kushindwa kutumia vema nafasi ambazo walizotengeneza.

Yanga jana walipoteza mchezo wa tatu kwenye ligi kuu baada ya kukubali kufungwa bao 1-0 lililofungwa na Haruna Shamte aliyepiga faulo iliyozama mojakwamoja ndani ya lango.

Kamusoko amesema hakuna kingine ambacho kimewaponza kupoteza mchezo wao zaidi ya ushindani pamoja na bahati kutokuwa kwao kwenye mchezo huo.

"Haikuwa bahati yetu kupata matokeo chanya kwani tumecheza vizuri na tumetengeneza nafasi nyingi tukashindwa kuzitumia kwenye mchezo wetu.

"Bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye michezo yetu inayofuata hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema Kamusoko.

Yanga ni vinara wa ligi kwa sasa wakiwa na pointi 67 baada ya kucheza michezo 28 wamepoteza michezo mitatu na kutoa sare michezo minne.

3 COMMENTS:

  1. kweli lazima iwepo sababu kwasababu yanga sio timu ya kufungwa na timu yoyote. Endeleeni kujidanganya na kudanganya

    ReplyDelete
  2. Sababu ni kocha hakuambatana na timu ile abaki dar kuwapa vita mchongo wa kuifunga Simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kocha asingeweza kwenda Iringa na kusafiri kesho yake,na Yanga wameshacheza mechi zaidi ya tatu na kushinda bila kocha kuwepo

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic