MCHEZAJI SIMBA KUCHUKUA NAFASI YA DANTE STARS
Wakati veki wa Yanga Andrew Vincent akiwa jijini Dar es Salaam baada ya kuachwa kutokana na kuwa majeruhi, inaelezwa nafasi yake itachukuliwa na beki kiraka wa Simba, Erasto Nyoni katika kikosi cha timu ya taifa.
Tayari kikosi cha Stars kimeshatangazwa na Kocha Emmanuel Amunike huku akiliacha jina la Nyoni ambaye alikuwa majeruhi.
Lakini hivi sasa zilizo chini ya kapeti zinasema Nyoni ataingizwa ndani ya kikosi hicho kujiandaa na mechi ya kufuzu kuelekea AFCON dhidi ya Uganda, mechi itakayopigwa Machi 24 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Nyoni ametajwa kuchukua nafasi hiyo baada ya kupona majeraha yake ambayo aliyapata katika mashindano ya Mapinduzi wakati akiwa kibaruani kuitumikia Simba.
Beki huyo hivi sasa tayari ameshaanza mazoezi mepesi na anaweza kuwa sehemu ya mchezo wa kesho dhidi ya AS Vita utakaopigwa kesho Jumamosi.
0 COMMENTS:
Post a Comment