March 16, 2019


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kuwa chochote kibaya kitakachompata Kocha wake Mkuu, Mwinyi Zahera, watawahusisha watani zao wa jadi Simba.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema hayo huku akiwataka Simba wajitokeze hadharani kukanusha ambayo wamekuwa wakimhusisha nayo Zahera.

Jana Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema Kocha wa Yanga amekuwa na ukaribu na viongozi wa AS Vita kwa ajili ya kuiharibia Simba mipango ya kushinda mchezo wao wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Manara alieleza kuwa Zahera amekuwa akitembea nao kwa ukaribu huku akiiacha timu yake ya Yanga ikisaifiri kuelekea Iringa huku akiaga kuwa atasafiri kwenda Congo ingawa mpaka sasa hajaondoka nchini.

"Kauli za kichochezi dhidi ya kocha Zahera Mwinyi, Wanayanga wote tuamini kuwa jambo lolote baya litakalo mpata Kocha wetu basi Uongozi wa Simba unahusika.

Kama la wajitokeze hadharani kukanusha au kuzikemea kauli hizo. Soka ni mchezo wa kiungwana, vipi wengine waugeuze kuwa sehemu ya uchochezi na ubaguzi." amesema Ten.

6 COMMENTS:

  1. Wewe ndio mchochezi mkubwa.Kocha gani unazungumzia?Kocha ambaye ameikacha timu yetu inayocheza leo Iringa na kubaki Dar ili aunge mkono timu iliyotoka nyumbani kwao Congo!!Awasaidie bila kujali kwamba timu inacheza leo?
    Uaminifu wake upo wapi Yanga au As Vita?
    Halafu baada ya kumwajibisha Dismas unauunga mkono ujinga?
    Kweli umaskini ni maradhi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha hizo Yanga hata bila Zahera Iringa tutashinda acha akawaharibie Mikia.

      Delete
  2. HUYU MSEMAJI WA VYURA NI SHOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOGA NINI?

    ReplyDelete
  3. Ndio ni shogabosho kwani hujui au mpaka umegewe?

    ReplyDelete
  4. kocha Zahera yuko DRC na majukumu ya timu ya Taifa ambayo iko Dar kucheza na Simba

    ReplyDelete
  5. Mijinga haina akili.Haya mmepigwa kote kote. Binti mdogo kaolewa Iringa nä binti mkubwa kaolewa kwa Mkapa. Harusi zote zimejibu. Sherehe zinaendelea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic