March 7, 2019







Na Mwandishi Wetu
MWALIMU wa Shule ya Atlas ya Madale jijini Dar es Salaam, Renovatus Philbert amefanikiwa kushinda Shilingi Milioni 26, 659, 362 za Multibet ya SportPesa.


Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Philbert alisema kuwa huo ni ushindi wake wa pili kuushinda ndani ya mwezi huu baada hivi juzi kushinda Shilingi Milioni 10.

Philbert ambaye ni mkazi wa Tegeta, Dar alisema kuwa baada ya ushindi huo amepanga kuzitumia pesa hizo alizozipata kwa kununua kiwanja na kuanza ujenzi wa nyumba atakayoishi yeye na familia yake.


Aliongeza kuwa, mwaka tatu kwake tangu ameanza kubashiri na SportPesa na kujishindia mara kadhaa pesa baada ya ubashiri wake mzuri aliokuwa anaufanya wa mechi mbalimbali.

“Mimi ni mwalimu wa shule ya Atlas ya Madale ambaye tofauti na kazi yangu hiyo ya ualimu mara nyingi nimekuwa nikibashiri kupitia SportPesa.


“Kampuni ya SportPesa ni tofauti na nyingine ambazo nilizowahi kucheza nayo, yenyewe ukishinda kwa usahihi katika mechi zako, basi ndani ya dakika ya kumi unatumiwa fedha zako kupitia simu yako ya mkononi.


“Hivyo, nimepanga kuendelea kubashiri matokeo na SportPesa ambayo nimekuwa nikiiamini katika malipo yao ya pesa baada ya ushindi, hivyo niwasahauri vijana wabashiri matokeo na SportPesa,”alisema Philbert.

Kwa upande wa SportPesa Mkurugenzi wa Uendeshaji, Luca Neghesti alimpongeza Philbert kwa ushindi huo wa Multibeti huku akimtaka kuendelea kubashiri zaidi kupitia SportPesa ili ajishindie pesa zaidi.


“SportPesa imepanga kuboresha maisha ya Watanzania wote watakaobashiri na SportPesa, kikubwa wanachotakiwa ni kubashiri kwa usahihi pekee ili wafanikiwe kujishindia mabilioni na wafanikiwe kutimiza ndoto zao.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic