Mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba na Taifa Stars, Mohamed Mwameja amesema kueleka mechi ya Simba na AS Vita katika Ligi ya Mabingwa Afrika, kuwa kila mmoja ana nafasi ya kupata matokeo.
Kipa huyo aliyetamba zaidi miaka ya nyuma akiwa na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania amesema hayo kutokana na ubora wa timu zote mbili haswa Vita ambao wana uzoefu zaidi na mashindano haya.
Mwameja amefunguka kuwa kila mmoja ataweza kupata kutokana na maandalizi ya ambayo kila timu imeyafanya.
Ombi lake kwa Simba
Mwameja anaamini Simba kupata matokeo lakini kama hawataruhusu kufanya makosa ambayo yamekuwa yakifanyika katika mechi za ugenini.
Moja ya makosa hayo ni Mwameja ameyataja ni kuruhusu mabao ya mapema kitu ambacho kinaweza kuwaathiri Simba mchezoni.
Amewataka pia kupunguza udhaifu katika nafasi ya ulinzi ili kuwabana Vita ambao ni wakamiajia wa kufunga halikadhalika kuepuka mipira ya kona.
"Mechi itakuwa ngumu japo kila timu inaweza kupata matokeo.
"Ni vema Simba wakaongeza umakini kwenye safu ya ulinzi ili kutoruhusu mabao ya mapema ambayo yanaweza kuwaharibia malengo yao kwenda hatua inayofuata.
"Na mechi hii ipo wazi kutokana na kila timu kutaka matokeo japo Simba wanhitaji zaidi kushinda."
Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wadau pamoja na mashabiki wa soka hapa nchini itapigwa majira ya saa 1 za usiku Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
mechi saa moja usiku lini? we mwandishi umesoma kweli????????
ReplyDeleteUwe unafanya utafiti kwanza kabla haujakurupuka kutoa shutuma kwa mwandishi,nadhani wewe ndo utakuwa hujasoma au wakati unapost mawazo yako ulikuwa umetoka kuamka maana sote tunajua kuwa mechi itapigwa kuanzia mida ya saa moja usiku kwa mujibu wa maagizo ya CAF
Delete