KIKOSI cha Simba leo kinashuka Uwanjani kumenyana na Ruvu Shooting mchezo wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Taifa.
Simba wanaingia Uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kuwapa kichapo cha mabao 5-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Ruvu Shooting hivi karibuni, katika mechi 8 zilizopita imeshinda mechi mbili, sare 5 na kupoteza moja. Wakati Simba imeshinda mechi 7 za ligi kuu zilizopita.
Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema hana mashaka na kikosi chake atawashangaza wengi kwa kupata matokeo chanya.
"Hakuna namna tunahitaji matokeo chanya kwenye mchezo wetu kikubwa ni kuona namna ambayo tutabeba pointi tatu kwa wapinzani wetu Simba," amesema Bwire.
0 COMMENTS:
Post a Comment